Tuesday, April 1, 2014

BARAZA LA MADIWANI LA MJI KOROGWE LAUPOKEA KWA MIKONO MIWILI MPANGO TIBA KWA KADI (TIKA)


Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani katika kupitisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha mwisho kimefanyika Machi 29, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akitoa maelezo machache juu ya TIKA. Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia kwa makini.

Waheshimiwa Madiwani wakitoa misimamo yao.
Waheshimiwa Madiwani walipata wasaa wa kuhoji kabla ya kukubali kwa mikono miwili mpango wa Tiba kwa Kadi.
Waheshimiwa Madiwani walipata wasaa wa kuhoji kabla ya kukubali kwa mikono miwili mpango wa Tiba kwa Kadi.
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa ufafanuzi jinsi sheria za TIKA zinavyofanya kazi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale akisoma sheria za uanzishwaji wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ili zibarikiwe na Baraza la Madiwani ambapo kwa kauli moja wameubariki mpango huo na sasa tika itaanza kupigiwa debe na watu wajiunge ambapo jana katika kikao cha wadau jumla ya milioni 1.3 zilichangwa.

No comments:

Post a Comment