Tuesday, July 29, 2014

MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao hatari a majambazi wapatao kumi (10) mmoja wao akiwa ni mwanamke anayeshiriki kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi.  Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini D’Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa D’Salaam vinalindwa kikamilifu.  Katika msako huo watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 8 kama ifuatavyo.
    1. SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
    2. SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
    3. BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
    4. BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670
Na risasi 6 ndani ya magazine.
    1. S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
    2. MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
    3. BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
    4. SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
    5. SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako

Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
  1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE  miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
  2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
  3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
  4. SAID S/O FADHIL MLISI miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
  5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
  6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
  7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
  8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
  9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
  10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilalakala
Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.  Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.

Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.  Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.  Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kupekua majalada yao ya kesi mbali mbali.

No comments:

Post a Comment