Tuesday, July 29, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL FITRI 2014.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-
  • Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.

  • Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida (GD), askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero. Wote hawa wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike. Kwa mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa pasi na ajizi.

  • Zitakuwepo doria za Miguu, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.

  • Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya Idd El FITRI katika ngazi ya familia au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea.

  • Aidha kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jeshi la Polisi limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi viwango vya kiusalama.

  • Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili hatua zichukuliwe kwa haraka.

  • Madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wasiwe walevi, magari au pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo ni marufuku.

  • Aidha, Kikosi cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria kwenye fukwe za Bahari na maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam. Patakuwepo Helkopta ya Jeshi la Polisi ikifanya doria kuzunguka jiji la Dar es Salaam na askari wa Kikosi cha Mbwa na Farasi nao watahusika na doria.

  • Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya Polisi vya muda vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani

  • Aidha, kwa urahisi wa mawasiliano wananchi wasisite kutoa taarifa za uhalifu kwa namba muhimu za simu zifuatazo: 
    1. RPC ILALA:  Mary Nzuki – SACP 0754 009 980 / 0754 339 558
    1. RPC TEMEKE: Kihenya wa Kihenya SACP 0715 009 979/ 0754 397 454
    2. RPC KNDONI: Camillius Wambura ACP  0715 009 976 / 0684 111 111


“NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL HAJI 2014”.


S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment