Tuesday, August 26, 2014

BARA BARA ZA AICC KIJENGE ZINATISHA KWA UBOVU






Wananchi wa kata ya them, eneo la magorofa ya aicc wamelalamikia ubovu wa barabara za ndani, kuzunguka magorofa hayo ,ambazo zina zaidi ya miaka ya miaka 16 sasa bila ukarabati

wananchi hao wamelalamikia uongozi mzima unaosimamia barabara hizo zinazoingia na kutoka katika nyumba hizo zinazomilikiwa na taasisi kubwa, inayomiliki , ukumbi  mkubwa wa mikutano ya kimataifa na mashuhuri wa Aicc jijin Arusha.

Pamoja na ubovu wa barabara hizo ,tayari umejitokeza usumbufu kwani magari ya mizigo yamekatazwa kupita katika barabara hizo ,eti lengo ni kuhifadhi barabara hizo chakavu ziliyojaa mashimo kama mahandaki ,kwa kuweka mageti na walinzi kila kona.

Walinzi hao nao,  wameanzisha mradi wao ,wa kujikusanyia shiling elfu moja moja, kutoka kwa madereva wanaotaka kupita na magari yenye mizigo hata ile isiyozidi nusu tani.

Wananchi na wakazi wa eneo hilo wamepania kufuatilia kwa kina  suala hilo,kwa uongozi  ili kujua ufafanuzi  na suluhusho la barabara hiyo, iliyotelekezwa bila ungalizi.

Kutoka them jijin Arusha ni Gasper sambweti wa g sambweti blog

No comments:

Post a Comment