Tuesday, August 5, 2014

KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WAWILI, BASTOLA MBILI NA RISASI 14

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia majambazi wawili kwa kutuhuma za kujihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani. 

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 30/07/2014 huko Makumbusho Kijitonyama, kufuatia msako makali unaoendelea wa kuwasaka kisha kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha na makosa mengine. 


Walipopekuliwa nyumbani kwao walikamatwa na Bastola mbili moja ni GROCK17 yenye namba B019259 iliyotengenezwa nchi ya Jamhuri ya CZECH ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine. Nyingine ni Bastola aina ya CHINESE iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi moja ndani ya magazine.


Watuhumiwa waliokamatwa ni hawa wafuato:
  • FREDY S/O STEVEN, Miaka 25, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kiwalani.
  • IRENE D/O NYANGE, Miaka 36, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kijitonyama, uchunguzi unakamilishwa na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment