Tuesday, August 5, 2014

WANAWAKE WATATU WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA MTANDAO HARAMU NA NYARA ZA SERIKALI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM linawashikilia wanawake watatu kwa kosa la kujihusisha na mtandao haramu wa nyara za Serikali. Mnamo tarehe 23/07/2014 huko eneo la Mbagala Mission Polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa eneo hilo lina watu wanajihusisha na biashara ya nyara za serikali. 

Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata WEMAEL D/O MSHANA na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vipande sita vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za Kimarekani 30,000 (Dolla elfu thelathini) sawa na shilingi za kitanzania 49,750,000/= (milioni arobaini na tisa mia saba hamsini elfu) ambao ni sawa na tembo wawili waliouawa.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa anashirikiana na watuhumiwa wengine ambao ni UPENDO D/O MSHANA, Miaka 33, na STELLA D/O DANIEL, Miaka 17, Mwanafunzi wa Chuo cha Genessis cha Mtoni kwa Azizi Ali ambao nao wamekamatwa.
Uchunguzi zaidi unafanyika kwa kushirikiana na Idara ya wanyama pori ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment