Monday, September 15, 2014

KINANA AKAGUA SHAMBA LA MIKOROSHO 19270 ILIYOHARIBIKA KATIKA KIJIJI CHA MAGAWA, MKURANGA NA KUWAAHIDI KUWASAIDIA WAKULIMA WA ZAO HILO KUPATA FIDIA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia moja kati ya miti 19,270 ya korosho iliyoharibika  alipokwenda kukagua shamba la hekali 1000 katika Kijiji cha Magawa wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akiongoza kukagua shamba la mikorosho iliyoharibika na kuwafanya wananchi wa Kijiji cha Magawa kuwa masikini.
 Kinana akizungumza na wakulima wa zao hilo katika Kijiji cha Magawa, ambapo aliahidi suala lao hilo kulipepeleka kwa Waziri Mkuu, ili wapatiwe fidia na serikali kama walivyopatiwa wafugaji waliofiwa na mifugo yao katika baadhi ya ikoa nchni.
 Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rufiji,na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  mkoani Pwani, alipowasili katika wilaya hiyo kuanza ziarfa ua kuimarisha uhai wa chama.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rufiji,na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  mkoani Pwani, alipowasili katika wilaya hiyo kuanza ziarfa ua kuimarisha uhai wa chama.
 Nape Nnauye akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu leo katika Mji wa Ikwiriri
 Kinana akisaidia kuranda mbao baada ya kufungua Tawi la Vijana wajasriliamali la Mayuyu Mjini Utete, Wilayani Rufiji leo
 Kinana na Nape wakiangalia viti walivyozawadiwa na kikundi hicho cha VIJANA
 Kinana akikagua jengo la Ofisi ya Wilaya ya Rufiji baada ya kulizindua mjini Utete leo
 Kikundi cha hamasa cha CCM Wilayani Rufiji, wakicheza ngoma katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kinana mjini Utete leo
 NNape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Utete leo
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiwili, Kata ya Utete,Sudi Nassoro akijeleza mbele ya Kinana jinsi wanavyosuluhisha migogoro dhidi ya wafugaji na wanakijiji katika kkutano huo.
 Mzee Shamte Ungusa (71), mkazi wa Utete Mjini, akilalamika  mbele ya Kinana jinsi serikali ilivyowasahau kwa kipindi kirefu kuwajengea barabara ya lami kutoka Nywamwage hadi mjini Utete ambapo ni makao makuu ya Wilaya ya Rufiji.
 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utii mbele ya Kinana baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho katika mkutano huo
Kinana akaikagua jengo jipya la uzazi la akina mama katika Kijiji cha Nyamwage.
Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Juma Abeid Diwani wa Kata ya Magawa wilayani Mkuranga wakati alipotembelea shamba la Mikorosho lenye hekari 1000 ambapo mikorosho inayokaribia elfu 20 imeharibika vibaya baada ya kupata ugonjwa unaonyausha mikorosho hiyo , Diwani huyo amesema wananchi wa kata hiyo wako katika hali mbaya kwakuwa zaidi ya miaka minne sasa hawajavuna chochote na maisha yao yanazidi kuwa mabaya, Katibu Mkuu Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- 2 
Mmoja wa wapiga ngoma wa kikundi cha ngoma cha mjini Utete akipiga ngoma huku akiwa amebeba mtoto wake mdogo na mtoto wake mwingine akiwa amekaa pembeni. 15 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo. 17 
Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mh. Nurdin Babu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Utete leo 18 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Utete wakati wa mkutano wa hadhara uliofnyika mjini Utete.  21 
Baadhi ya wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama 23 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dr. Onesmo Mambosho Mganga Mfawidhiwa wa kituo cha afya cha Nyamwage.

No comments:

Post a Comment