Monday, September 15, 2014

MAJAMBAZI SUGU WAWILI WAKAMATWA NA SMG JIJINI DAR ES SALAAM




Jeshi la Polisi Kanda Maalum limeendelea na oparesheni zake kuwatafuta na kuwakamata majambazi wote wanaofanya uhalifu wa kutumia silaha na uhalifu mwingine ili sheria ichukue mkondo wake. Katika oparesheni hiyo yamekamatwa majambazi wawili kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia katika matukio ya ujambazi.

Kabla ya kukamatwa kwa bunduki hiyo watuhumiwa walikuwa wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika maduka ya MPESA na TIGO PESA yaliyopo maeneo ya Sinza Madukani. Majambazi hao waliahirisha kufanya tukio baada ya kushtukia mtego wa polisi.  

Mnamo tarehe 10/09/2014 majambazi hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa kuwa yamejipanga kufanya tukio la uhalifu maeneo ya YOMBO DOVYA na kisha kuweka mtego katika nyumba ya ASIA D/O ALLY KASHINDE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 iliyopo maeneo ya Yombo Makangarawe (M) wa Kipolisi wa Temeke. Baada ya kuwakamata majambazi hao walipekuliwa katika chumba wanacholala ndipo ilipopatikana silaha aina ya SMG yenye namba IC 5740 ikiwa na risasi 07 ndani ya magazine. Bunduki hiyo imekatwa mtutu na kitako. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuwezesha kuwakamata wengine wanaoshirikiana katika genge hili la ujambazi.

Majina ya watuhumiwa wa ujambazi waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1.   KHAMIS S/O AMBA, Miaka 40, Mkazi wa Yombo Makangarawe.
2.   OMAR S/O KHAMIS, Miaka 43, Mkazi wa Masasi Nyasa Mtwara

No comments:

Post a Comment