Monday, September 15, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ITAKAYOTOLEWA NA KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM SULEIMAN KOVA TAREHE 15, SEPTEMBA 2014 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA KANDA MAALUM





 UTANGULIZI
Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam ina utaratibu wa kufanya mazungumzo na wananchi kwa kupitia vyombo vya habari vya aina mbalimbali kwa lengo la kuwapasha habari wananchi kuhusu hali ya usalama jijini na hatua zinazochukuliwa na Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam katika kukabiliana na changamoto za uhalifu jijini na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi husika.
Katika kipindi cha wiki mbili tangu tulipokutana mara ya mwisho yametokea  matukio ya uhalifu ya hapa na pale ambayo wananchi ambao ni walaji wa huduma za ulinzi na usalama wanatakiwa kupewa taarifa ili kwa pamoja tushirikiane kupunguza uhalifu jijini au kuutokomeza kabisa.

TAARIFA YA MAFANIKIO KATIKA UTENDAJI
Matukio yaliyojitokeza katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ni haya yafuatayo


OPERATION MALUM YA KUZUIA KUPAMBANA NA MATISHIO YA UHALIFU KUFANYIKA D’SALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaanzisha operesheni maalum ya kupambana na vitendo mbali mbali vya uhalifu ambayo vimejitokeza na kuashiria uvunjifu wa amani na kuleta tishio kwa wakazi wa D’salam.
Matukio yaliyojitokeza kwa matishio ni kama yafuatayo:-
1.   Ujambazi wa kutumia silaha
2.   Dawa za kulevyaa za viwandani na mashambani
3.   Majambazi wanaoteka na kufanya uhalifu dhidi ya watu wanaosafirisha fedha taslim kiholela
4.   Majambazi wanaovizia katika mabenki na maduka ya kubadilishana fedha (Bureau De Change)
5.   Vikundi vinavyojihusisha na itikadi kali kwa kutumia mwavuli wa Dini, siasa au wahalifu wanaofanya vitendo vinavyoashiria na kujielekeza katika kufanya ugaidi.
6.   tutapambana na kero ambazo ni vyanzo vya uhalifu ambavyo ni maeneo yanayojihusha na kusambaza na kuuza dawa za kulevya, upishi wa pombe haramu ya gongo, baa na grocery yanayokesha na katika pamoja na wateja wao wakilewa kucha na wale wanaopiga mziki usiku katika mtaa bila kujali maisha au mapumziko kwa raia wengine wanaoishi jirani.
Operesheni hiyo imezingatia kumbukumbu za uhalifu ambazo zimeanza kujitokeza wakati wa mchana na usiku ambapo kama mwenendo huo hautadhibitiwa hali ya utulivu katika jiji la D’Salaam utavurugika na wananchi wataanza kuishi katika hali ya hofu.  Aidha yapo mawasiliano ya karibu kati ya Polisi Kanda Maalum na Makamanda katika mikoa ya mipakani ili kuhakikisha kwamba silaha zote zinazoingia D’Salaam hazivushwi kiholela kwa njia za panya katika mikoa hiyo na hatimaye kutumika kwa uhalifu katika jiji la D’Salaam.
Operesheni hii kali ya aina yake inataendeshwa kwa awamu tatu hadi mwishoni mwa mwaka huu.  Tunatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili mafanikio makubwa zaidi yapatikane dhidi ya uhalifu.
MTANDAO WA WAHALIFU WANAOTUMIA TEKNOLOJIA YA  MAWASILIANO (IT) WAKAMATWA JIJINI DA ES SALAAM

        Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam limewakamata watu wawili wanaojihusisha na mtanda wa uhalifu kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano (IT) ambapo taarifa za kiintelijensia zilionyesha kwamba lengo lao ni kuwasaidia wahalifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na wale wa kutumia silaha. Pia imebainika kwamba watuhumiwa hawa huwasaidia watu walioiba simu kwa kubadilisha kumbukumbu zao ili wasiweze kukamatwa na Polisi.

Watuhumiwa hawa walikamatwa tarehe 11/09/2014 huko Kariakoo katika mtaa wa Agrey wakijifanya ni mafundi wa kawaida wa simu ambapo wamesomea teknolojia ya mawasiliano (Information Technology) katika vyuo vilivyopo jijini Dar es Salaam kwa sasa ni mafundi wa simu za mikononi ambao hujihusisha na vitendo vya KUFLASH SIMU, KUFUNGUA PASS WORD, na kupoteza IMEI NAMBA za simu wanazoletewa na wahalifu kwa lengo la kubadilisha utambulisho (IDENDIFICATION) na uhalisia wa simu husika.
Majina ya watuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1.   EDSON S/O KENNEDY NDEIKYA, miaka 27, fundi simu mkazi wa Mabibo Kanuni.
2.   IBRAHIM S/O MUHDINI KASUKU, miaka 23, fundi simu, mkazi wa Keko Magurumbasi.

No comments:

Post a Comment