Tuesday, July 21, 2015

Milio ya risasi yatanda uchaguzi wa Burundi

Miripuko  na  milio  ya  risasi  ilisikika  katika  mji  mkuu  wa Burundi, Bujumbura, usiku  wa  jana   ambapo  watu wawili  wanaripotiwa  kuuwawa masaa  machache  kabla ya  vituo  vya  kupigia  kura  kufunguliwa katika  uchaguzi unaofanyika  leo.
Hali  ya  ukosefu  wa  utulivu  inakuja  kutokana  na wasiwasi  kuhusiana  na  juhudi  zenye  utata  za  Rais Pierre Nkurunziza  kutaka  kuchaguliwa  tena  kwa  kipindi cha  tatu, ambapo  waandamanaji  wamesema  nia  yake hiyo  inakiuka  katiba, ambayo  inaruhusu  ukomo  wa vipindi  viwili.
Vituo  vya  kupigia  kura  vimefunguliwa  leo  asubuhi kwa ajili  ya  uchaguzi  huo  ambao  unasusiwa  na  vyama vikuu  vya  upinzani  na  kutishia  kuitumbukiza  nchi  hiyo ya  Afrika  Mashariki  katika  ghasia  kubwa. Zaidi  ya  raia 160,000 wa  Burundi  wamekimbilia  nchi jirani, wengi wakisema  wanahofia  mashambulizi  ya vijana  wa  chama tawala  wanaojulikana  kama  Imbonerakure

No comments:

Post a Comment