Kisumu, Kenya —
Raila Odinga Junior ametambuliwa rasmi kama kiongozi mpya wa familia ya Jaramogi Oginga Odinga. Sherehe ya kitamaduni ya ‘liedo’, ikijumuisha nyimbo, ngoma za kienyeji na kunyoa nywele, ilifanyika nyumbani kwao Opoda kabla ya msafara kuelekea Kango ka Jaramogi.
Mheshimiwa Ruth Odinga, Mbunge wa Kaunti ya Kisumu (Woman Representative), alisema:
"Leo ni siku ya kumbukumbu na mwanzo mpya. Tunamuombea Junior hekima, ujasiri na uthabiti katika jukumu hili la kifamilia."











































