Wednesday, October 18, 2017

SERIKALI YA IRELAND YAWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 KUPAMBANA NA UKATILI WILAYANI MISUNGWI


SERIKALI ya Jamhuri ya Ireland kupitia Shirika la Maendeleo nchini humo limetoa msaada wa kiasi cha Uero 350,000 (zaidi ya milioni 700) kwa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwezesha mpango wa kujenga uwezo wa jamii na taasisi za Serikali ili kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata 10 wilayani Misungwi mkoani hapa.

Msaada huo umetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon,  aliye ambatana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini humo, Ruairi De Burca pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock, kwenye uzinduzi wa Mradi wa mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi.

Kata zilizo nufaika na mradi huo ni pamoja na Usagara, Idetemya, Kolomije, Igokelo, Misungwi, Mbarika, Misasi, Nundulu, Sumbugu na Mabuki walengwa watakaofikiwa moja kwa moja  144,744 na wengine 289,488 ambao watafikiwa kwa kupata elimu kutoka kwa wananchi wengine waliopata mafunzo.Mwanamke mmoja kati ya saba nchini Tanzania amebainika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hatua  ambayo inazidi kuchangia kupunguza nguvu kazi ya taifa.


Waziri huyo wa Mambo ya nje wa Ireland, Bwana Cannon amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali ikiwemo kupambana na vitendo vya Ukatili, Afya na Mfuko wa kusadia kaya masikini nchini (TASAF) ili kuleta mabadiliko katika Nyanja ya Uchumi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akikata utepe wa moja ya vijarida vya uelimishaji kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi, Mwanza, kushoto ni mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
"Ndiyo hiki"..........!
Oyeeeeeee......!!
Yaliyomo yamo?
Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock naye akizawadiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa kupambana na ukatili wa jinsia, uliofanyika kwenye viwanja vya Amani wilayani Misungwi, Mwanza, kushoto ni mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akifunguka mbele ya wananchi na kusanyiko.
Zaidi ya asilimia 40 ya Wanawake nchini (Tanzania) wamebainika kukumbwa na vitendo vya ukatili, hali ambayo haiwakumbi wanawake pekee bali pia wanaume, nao wameripotiwa kukumbana na vitendo hivyo vya ukatili nazo takwimu zikishindikana kupatikana ipaswavyo kutokana na wanaume hao kuona kama ni suala la aibu na fedheha kuripoti kwamba wametendewa ukatili.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewaonya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili akisema kuwa serikali haitosita kuchukuwa hatua kali kwa wahalifu hao. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Yasini Ally.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kivulini, Yasini Ally amema Wilaya Misungwi ilikuwa ikikabiliwa kiwango cha kutisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake kunyanyaswa na waume zao ambapo wamepambana  kwa kila hali hatimaye sasa wanashuhudia vitendo hivyo kupungua kwa kasi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

 
Awali kabla ya kuzindua mradi huo wa Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto unaoendeshwa na KIVULINI Waziri huyo ameshuhudia uzinduzi wa Zoezi la Uhawilishaji fedha katika kijiji cha Misungwi pamoja na kutembelea kituo cha Afya cha Misasi ambapo ameahidi Serikali yake itaendelea kuchangia katika utatuzi wa changamoto zake.

Kwa mjibu wa takwimu za Mwaka 2015/ 2016 zinaonyesha kuwa, vitendo vya ukatili wa kinjisia nchini ni asilimia 58 kitendo ambacho kimetajwa kuwa kinachangia shughuli za maendeleo katika jamii kusuasua.
Ngoma asili.
Jiografia ya eneo la uzinduzi.
Ngoma asili ikichukuwa nafasi kunako kusanyikoni.
Wadau walio na dhamana ya uelimishaji toka KIVULINI wakisikiliza kwa umakini yanayojiri kusanyikoni.
Utambulisho.
Ngoma inogile.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwilu Girls toka jijini Mwanza nao wameshiriki uzinduzi huo unao husika katika Ku-Chochea Mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo nchini Ireland, Ruairi De Burca akizawadiwa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon akiselebuka mangoma ya kisukuma sanjari na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.
Wanaharakati walipata fursa ya kueleza jinsi gani wanavyo sambaza elimu, shughuli zao, changamoto na ushauri.
Kisha nao wakapewa somo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulikia Maendeleo, Ciaran Cannon.
Dawati la Jinsia toka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likifanikisha adhma yake katika usaidizi wa kisheria, uelimishaji, kupambana na udhibiti wa vitendo vya ukatili kwa jamii.
Kivulini is a civil society organisation which works to improve women’s rights in Tanzania . Kivulini advocates for women’s and girl ’s rights in Tanzania by emphasising the prevention of Violence against women against women and girls. 

The Kiswahili word Kivulini means “in the shade”. It implies a place of safety, under a tree or otherwise, where people meet for discussions and offer support to one another. 

Kivulini was established in 1999 to create opportunities for community members to come together, talk, organise and work towards preventing domestic violence so that women and girls are able to enjoy their rights as stipulated in the Constitution of The United Republic of Tanzania, African Charter and various human rights conventions.

VISION

Kivulini’s vision is to see a community free from domestic violence where women’s rights are respected and valued. Kivulini’s mission seeks to achieve this vision by facilitating and enabling social, economical, and legal environment which guarantees women and girls the right to live in violence-free communities through self empowerment, advocacy and building an active social movement for change.

OBJECTIVES

Kivulini is committed to facilitate an enabling social, economical, and legal environment which guarantees women and girls the right to live in violence-free communities through self empowerment, advocacy and building an active social movement for change. 

To build momentum for the prevention of Violence Against Women and girls with emphasis on domestic violence against women and girls in the Lake Victoria Regions (Mwanza, Kagera, Mara and Shinyanga) and Singida by:

  1. Mobilizing communities to take action against Domestic violence
  2. Strengthening the capacities of local government and CSOs (including Kivulini)
  3. Advocating and influencing key local and national policies that empower and benefit women and girls.

WAZIRI KAMWELWE AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI MOSHI


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tenki la Maji la Njari.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira wakifungua bomba kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Mang’ana.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amkimtua ndoo kichwani mama kutoka Kijiji cha Mang’ana, akiashiria kutimiza lengo la Serikali ‘‘kumtua mama ndoo kichwani’’ baada ya uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.
Msafara wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ukielekea kwenye Chanzo cha Maji cha Mang’ana katika uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa pongezi nyingi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) kwa kufanikiwa kutoa huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100 kwa Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Hayo aliyasema alipokuwa akizindua Mradi mkubwa wa Maji wa Manga’na, uliopo Kata ya Uru Kaskazini, utakaohudumia zaidi ya vijiji 11 katika Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Moshi Vijijini baada ya kupokea taarifa ya hali ya huduma ya maji katika Mji wa Moshi.

“Nawapongeza MUWSA kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya, kwa kuwa ndio lengo la Serikali, kuwa ifikapo mwaka 2020 maeneo ya vijijini huduma ya majisafi na salama ifikie asilimia 85 na mijini asilimia 95. Nyinyi leo hii mmeshavuka lengo hilo kwa Manispaa ya Moshi, kwa kweli nimefurahishwa sana na jambo hili na mnastahili pongezi nyingi’’, alisema Mhandisi Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe aliendelea kusema kuwa kwa kufanikiwa lengo hilo, mamlaka hiyo sasa itaongezewa maeneo mengine zaidi, ili kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wengine wa Moshi Vijijini ambao hawajafikiwa na huduma ya maji, na kuahidi kama Waziri mwenye dhamana ya maji atawatafutia fedha kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwelwe ameagiza halmashauri zote nchini, kuwa usifanyike ujenzi wowote wa miradi kabla ya kupata chanzo cha maji cha uhakika, ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji nchini.

Waziri Kamwelwe alisema ni ufisadi kutengeneza miundombinu ya maji, bila kuwa na chanzo cha uhakika cha maji. Sitakubali miradi ikamilike halafu isitoe maji, wakati umefanyika uwekezaji mkubwa wa fedha za Serikali. Hivyo, ni marufuku mradi wowote kukamilika bila kutoa maji.

Naye Mkurugenzi wa MUWSA, Joyce Msiru alisema katika taarifa yake kuwa mradi huo ni moja ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na mamlaka yake, ukiwa umegharimu zaidi ya Sh. bilioni 2 na utahudumia zaidi ya wananchi 34,000.

Mkurugenzi Msiru alitaja baadhi ya vijiji vitakavyohudumiwa na mradi huo kuwa ni Kariwa, Longuo, Njari, Rau, Okaseni na Msuni.

UKARABATI UWANJA WA NDEGE KIA KUKAMILIKA DESEMBA.


Serikali imesema ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu ambapo kwa sasa umefika zaidi ya asilimia Tisini. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elius Kwandikwa, mara baada ya kukagua ukarabati wa jengo la kupumzikia abiria na upanuzi wa maegesho ya ndege katika uwanja huo leo mkoani Kilimanjaro.

"Nimeridhishwa na ukarabati unaoendelea katika uwanja huu na nafikiri mmejionea wenyewe kazi inaendelea vizuri, hivyo naamini kutokana na hali hii kazi itakamilika hivi karibuni, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa ukarabati huo ambao pia umehusisha maboresho ya mfumo wa maji taka unalenga kuleta tija kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla kutokana na kuwepo ongezeko la abiria, huduma za kijamii na kibiashara.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kukarabati na kujenga viwanja vya ndege nchini ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga kwa wananchi wake lengo likiwa ni kuchochea fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati.

Kwa upande wake, Meneja Miradi wa KIA, Mhandisi Mathew Ndossi, amesema kuwa maegesho yatakapokamilika yatakuwa na uwezo wa kuegesha jumla ya ndege kubwa 11 kwa wakati mmoja badala ya 6 zinazoegeshwa sasa.

Ameongeza kuwa abiria wanatarajiwa kuongezeka kutoka laki nane kwa mwaka hadi kufikia milioni moja na laki mbili mara baada ya kukamilika kwa uwanja huo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua barabara ya Sakina - Tengeru (km 14.1) na barabara ya mchepuko ya Arusha (Arusha Bypass km 42.4) ambapo amesema kuwa kukamilika kwa barabara ya Sakina - Tengeru ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na wageni wanaoingia katika mkoa huo kwani kumepelekea kupungua kwa ajali na msongamano wa magari katika eneo hilo.

Ametoa wito kwa wananchi kuzitunza barabara na kutunza mazingira yanayozunguka barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi, Johny Kalupale, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kufanya kazi kwa ubora na kwa weledi ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuwajengea wananchi miundombinu bora na ya kisasa.

Awamu ya pili ya mradi huo sehemu ya barabara ya mchepuo ya Arusha (Arusha Bypass), inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inatarajiwa kukamilika mwakani na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 67.

Naibu Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi katika mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ambapo amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 
Meneja Miradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mhandisi Mathew Ndossi, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa (Mb), (Kushoto), upanuzi wa maegesho ya ndege uliofanyika uwanjani hapo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa (Mb), akikagua maboresho ya mfumo wa majitaka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alipofika uwanjani hapo kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati wa uwanja huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa (Kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja Miradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mhandisi Mathew Ndossi (Katikati), alipofika uwanjani hapo kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati wa uwanja huo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati katika jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Ukarabati huo umefika zaidi ya asilimia Tisini na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa,akifafanua jambo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Arusha, Mhandisi Johny Kalupale, alipokagua barabara ya Sakina – Tengeru (KM 14.1) na Barabara ya Mchepuko ya Arusha (Arusha Bypass KM 42.4) mkoani Arusha.
Muonekano wa Barabara ya Sakina – Tengeru (KM 14.1), mkoani Arusha,ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami. Kukamilika kwake kumesaidia kupunguza ajali na msongamano katika eneo hilo.
Muonekano wa Daraja la Nduruma lililopo katika barabara ya Sakina – Tengeru (KM 14.1), mkoani Arusha.

SERIKALI YA IRELAND YAPONGEZA TASAF KWA KUTEKELEZA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KWA MAFANIKIO. Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwa waziri wa Mambo ya nje wa Ireland namna shughuli za kuhawilisha fedha zinavyotekelezwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland akizungumza na Mkurugenzi wa TASAF,Ladislaus Mwamanga  wakati waliposhuhudia zoezi la kulipa ruzuku kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika wilaya ya  Misungwi,mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Ciaran akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Misungwi unaotekelezwa na TASAF namna walivyonufaika na huduma za Mpango huo.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongela akihutubia wananchi (hawapo pichani ) katika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland( aliyeketi kushoto )
 Waziri wa Mambo ya nje wa Ireland aliyeshika kipaza sauti akiwahutubia baadhi ya walengwa wa TASAF (hawapo pichani) katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (aliyevaa kofia) akiwa na mgeni wake waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland wakiwa na baadhi ya walengwa wa TASAF wakiwa na vyeti vya bima ya afya ya jamii waliyopata baada ya kujiunga na bima hiyo kwa kutumia  sehemu ya ruzuku ya  TASAF.NA ESTOM SANGA- MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Ireland bwana Ciar`an Cannon T.D amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za jamii na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi hususani wanaokabiliwa na umaskini .

Bwana Ciar`an ametoa pongezi hizo alipofanya ziara katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambako amekutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na kupata ushuhuda wa namna walivyonufaika na Mpango huo.

Baadhi ya Wananchi wanaonufaika na huduma za TASAF wamemweleza waziri huyo kuwa tangu waorodheshwe kwenye Mpango wameboresha maisha yao kwa huku wakijengewa misingi ya kujitegemea kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi,kuboresha na makazi yao .

Aidha baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wameeleza kuwa wamepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na afya katika kaya zao baada ya kujiunga na Mfuko wa Afya Jamii kwa kutumia fedha walizozipata kutoka TASAF na hivyo kuwapungizia mzigo mkubwa wa matibabu katika kipindi cha mwaka mzima,jambo ambalo wamesema limeboresha afya zao.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ireland amesema serikali yake imevutiwa na utekelezaji wa shughuli za TASAF na ili kuunga mkono juhudi hizo imepanga kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 7.3 katika kipindi cha mwaka huu ili kufanikisha shughuli za Mpango huo ambao ni miongoni mwa mipango mikubwa ya huduma za kijamii inayotekelezwa barani Afrika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Bwana John Mongela amewataka walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuzitumia vizuri fedha na huduma nyingine wanazopata kupitia TASAF ili kupambana na umaskini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali ya Ireland kwa kutambua jitihada za kupambana na umaskini na kuahidi kuwa Mfuko huo utaendelea kuzingatia maelekezo ya serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma kwa kaya za walengwa wa Mpango huo zipatazo milioni 1.1 nchini kote.

SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI


Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw. Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.


Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Mkoa huo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Bw. Seif Mkude (kulia) akielezea kuhusu utayari wa wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa kodi wakati wa Mkutano kati ya wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).


Mfanyabiashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo wa taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera katika kukuza Uchumi wa nchi baada ya Naibu Waziri huyo kufanyaziara ya kikazi Mkoani humo.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WFM


Benny Mwaipaja, KAGERA

Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.

Hayo yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).


Dokta Kijaji alisema kuwa wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, wakandarasi wamelipwa shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali wamelipwa Shilingi bilioni 38, watumishi wa umma wamelipwa Shilingi bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa shilingi bilioni 24.


Alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali na kwamba itaendelea kulipa madeni yote yaliyohakikiwa.

Dkt. Kijaji aliiambia Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera kwamba Serikali inatambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa kutokana na kulipa kodi zinazochangia kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali za jamii.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki katika biashara zao, kutoa stakabadhi wanapouza bidhaa na huduma huku wananchi wakiaswa kudai stakabadhi wanapofanya manunuzi ya aina yoyote na kuhakikisha kuwa stakabadhi hizo zinaonesha kiasi halisi walicholipia huduma na bidhaa walizonunua.

Akizungumza kwaniaba ya Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Seif Mkude, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyohamasisha na kushikia bango masuala ya kodi kwa manufaa ya Taifa.

Alisema kuwa wafanyabiashara wameridhika na namna kodi wanazolipa zinavyosimamiwa kikamilifu na kutekeleza miradi dhahiri ya maendeleo na kuahidi kuwa wataendelea kulipa kodi hizo ili kujenga uchumi wa nchi.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huku akiishauri Serikali kuondoa kero ndogondogo zilizotolewa na wafanyabiashara wakati wa mkutano huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro, aliwashauri wafanyabiashara hao kupanua wigo wa biashara zao ili waweze kunufaika na uwepo wa soko huru katika nchi zaidi ya nne zinazopakana na mkoa huo ikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, DRC Kongo, Kenya na nchi nyingine.