Taarifa kutoka
Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu
Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita.
Baada ya
kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali
inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia
jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake.
Makaziwe
amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri
duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka
kuingilia mambo yake binafsi Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku
vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndega aina ya Tai au
Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie
mzoga.
Wamevuka mipaka
ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona
sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa banangu? Ni
kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka
mipaka wanavyotaka, '' alisema Makaziwe
Mapema leo,
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alifutilia mbali ziara yake ya kwenda
Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika
hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj alisema kuwa hali yake imedorora zaidi
Mandela ambaye,
ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu
tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya
watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika
nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika
sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa
tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,''
alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka
kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika
Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.
Uamuzi wa Rais
Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa
kikanda kuhusu uekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea
kuzorota zaidi kulingana na mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Mike
Wooldridge.
No comments:
Post a Comment