Maduka
yamesalia kufungwa mjini Kampala Ugana kwa siku ya tatu leo huku
wafnyabiashara wakigoma kuhusiana na mpango wa serikali kusisitiza
viwango vya biadhaa zinazoingizwa nchini humo kuwa za juu.
Chama cha
wafanyabiashara hao kinasema kinapinga gharama wanayotozwa ikiwa bidhaa
wanazoingiza nchini humo sio za viwango vya juu. Malipo hayo ni kodi
iliyoanza kutozwa na serikali hivi karibuni ambayo inagharamia
kuchunguzwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo
Wanatak serikali ikome kuwatoza ushuru huo kwani wafnyabiashara tayari wanatozwa kodi ya juu.
Duru zinasema
kuwa vuguvugu la upinzani linatarajiwa kujiunga na maandamano hayo, na
kuwa polisi wamedhibiti hali ya usalama mjini Kampala.
Mwandishi wa
BBC mjini humo Catherine Byaruhanga anasema kuwa polisi huenda wakavunja
maandamano hayo kwa kuhofia otovu wa usalama.
Waziri wa
biashara, Amelia Kyambadde, ameelezea wazi kuwa Uganda inashinikizwa na
wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa iweze kutekeleza vikwazo
vya kuhakikisha kuwa bidhaa zinzoingizwa nchini humo ziwe za hali ya
juu.
Kodi hiyo
inalenga kuondoa uwezekano wa wafanyabiashara kuingiza biadhaa ghushi
nchi humo swala ambalo Uganda inatuhumiwa kutokuwa maakini nalo katika
kulitokomeza.
Wafanyabiashara
wanapaswa kuingiza nchini humo bidhaa za hali ya juu kutoka kwa
watengezaji wanaojulikana na ambao wako kwenye orodha inayojulikana kwa
mataifa ya Afrika Mashariki, ingawa wanasema kuwa gharama inayopaswa
kulipwa kwa hilo kufanyika ni ya juu zaidi.
No comments:
Post a Comment