Wednesday, June 6, 2012

Hali ya Mubarak yaendelea kuwa mbaya

Hali ya kiafya ya Hosni Mubarak imeendelea kuzorota tangu rais huyo wa zamani wa Misri alipowekwa gerezani Jumamosi iliyopita na huenda atahimishwa hospitali nje ya jela anakozuiliwa.

 Maafisa wa usalama wamesema kuwa Mubarak alisaidiwa kupumua kwa  kutumia mitambo mara tano katika muda wa saa za hivi karibuni na madaktari wanaomtibu wamependekeza ahamishiwe hospitali ya kijeshi, au arejeshwe katika hospitali alikokuwa kabla ya kuhukumiwa.


 Duru za usalama zimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa maafisa wa kamati ya matibabu kutoka wizara ya mambo ya ndani walimtembelea hospitalini na kusema kuwa amepata matatizo kadhaa ya moyo na kwamba hali yake inazidi kuwa mbaya. Shirika la habari la taifa NEMA limesema kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani anasumbuliwa na matatizo ya mapigo ya moyo pamoja na shinikizo la damu mwilini.

No comments:

Post a Comment