Wednesday, November 7, 2012

Matokeo yaanza kutolewa Marekani



Rais Obama na wafuasi wake
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.

Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko mbele ya  ya Romney kwa kura 9
      172
OBAMA
163
ROMNEY

    No comments:

    Post a Comment