Nchini Tanzania, chama tawala CCM kimekamilisha mchakato wa kuunda safu
ya uongozi wake kwa kuteua wajumbe wa kamati kuu baada ya kushindwa
kufanya hivyo Novemba mwaka jana.
Miongoni mwa wajumbe wa kamati kuu ni waziri mkuu mstaafu na katibu mkuu
wa zamani wa Umoja wa Afrika Dk. Salim Ahmad Salim. Wakatà huo huo,
majina makubwa yanayotajwa kuwa na nia ya kuwania urais mwaka 2015
yakiwemo ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, waziri wa mambo ya Nje
Bernard Membe na Spika wa zamani Samuel Sitta wote wameachwa nje. Iddi
Ssessanga amezungumza na mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya
kisiasa nchini Tanzania, Maggid Mjengwa kuhusiana na muundo wa safu hii
mpya.
No comments:
Post a Comment