Sunday, June 16, 2013

Dk Shein aelekea Uingereza, awashukuru Madaktari wa Kichina


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na mkewe, Mama Mwanamwema Shein, wakiagana na Viongozi mbali mbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakiondoka nchini jana kuelekea  Uingereza kwa safari Maalum ya wiki mbili. (Picha na ramadhan Othman, Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein, wakiagana na Viongozi mbali mbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,wakiondoka nchini  leo kuelekea Uingereza kwa safari Maalum ya wiki mbili.


Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar   
                                                                                                           
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeeleza kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na madaktari kutoka nchini China ambao wamekuwa wakija kufanya kazi hapa nchini kila baada ya miaka miwili tangu Zanzibar kupata uhuru Januari 12, 1964 hatua ambayo imeweza kuimarisha sekta ya afya.


Akizungumza na Madaktari kutoka China wanaofanya kazi zao hapa nchini ambao walifikia Iklu mjini Zanzibar kwa ajili ya kumaga baada ya kumaliza muda wao wa kazi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alitoa pongezi kwa niaba ya wananchi na Serikali kufuatia huduma nzuri wanazozitoa madaktari hao.

Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar inajivunia uhusiano na ushirikiano uliopo kwa muda mrefu kati yake na China ambao umeipelekea nchi hiyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya afya kwa kuleta madaktari.

Alieleza kuwa ni miaka 49 hivi sasa tokea Mapinduzi matukufu ya Janurai 12, 1964 yafanyike, China imekuwa ikileta madaktari ambapo tayari timu zipatazo 24 za madaktari kutoka nchini hyumo zimeshawasili hapa Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa huduma zinazotolewa na madaktari hao zimekuwa zikipendwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Unguja na Pemba.

Aliewaeleza madaktari hao kuwa mbali ya changamoto kadhaa zilizowakabili wakati wakiwa nchini katika utowaji wao wa huduma, madaktari hao wameweza kustahamili na kufanya kazi zao kwa ufanisi na ubora zaidi.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alitoa pongezi kwa uongozi wa nchi hiyo chini ya Rais  wake Mhe.  Xi Jinping, kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika mazungumzo yao waliyofanya  hapa Tanzania na huko nchini China hivi karibuni.

Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeweka mikakati maalum katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini na juhudi za China kuendelea kuiunga mkono Zanzibar zitaendelea kuleta mafanikio zaidi.

Madaktari hao walioongozana na Balozi Mdogo wa China anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Bibi Chen Qiman  na kusifu ukarimu pamoja na mashirikiano waliyoyapata madaktari hao katika kipindi chote cha miaka miwili waliyofanya kazi hapa Zanzibar.

Katika risala yao madaktari hao, walimueleza Dk. Shein kuwa wamevutiwa na kufarajika sana kwa mashirikiano waliyooneshwa na Serikali pamoja na wananchi wote wa Zanzibar.

Madaktari hao ambao tisa wanafanya kazi zao katika hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba na 12 wapo katika hopsitali ya Mnazi Mmoja, walieleza kuwa katika kipindi chao chote cha kazi cha miaka miwili wameweza kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na mashirikiano waliyoyapata.

Madaktari hao walieleza kuwa katika muda wao wote wa kazi walifanya kazi bega kwa began a madaktari wa Zanzibar.

Sambamba na hayo, Madaktari hao walimuhakikishia Dk. Shein kuwa wanarudi nyumbani lakini watahakikisha wanaitangaza Zanzibar kiutalii na kuwataka ndugu, marafiki, wanafamilia na wananchi wa China kuja kuitembelea Zanzibar kutokana na utajiri wa vivuti vya kitalii vilivyopo.

Walieleza kushuhudia kwao jinsi Zanzibar ilivyopata mafanikio katika kutekeleza Dira ya 2020 na kutekeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA)  kwa  kuimarisha miundombinu ya mawasiliano, usafiri na sekta nyenginezo.

Mbali ya mashirikiano mazuri waliyoelezea kuyapata wakati walipokuwa hapa nchini, madaktari hao walieleza kuwa  walitumia muda wao mkubwa katika kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar usiku na mchana na hata siku za mwisho wa wiki ambazo ni mapumziko wao walizutumia kwa kwenda vijini kutoa huduma za afya.

Madaktari hao kutoka China ambao wanamaliza muda wao kwa awamu hii jumla yao ni 21 ambao walianza kufanya kazi hapa nchini tokea June 2011 ambapo .

No comments:

Post a Comment