Saturday, June 15, 2013

KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI TANAPA CHAHITIMU MAFUNZO RUAHA NATION PARK.



1

Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za Taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kando kando ya Mto Ruaha, wakipewa mafunzo hayo na Wakufunzi,Martin Mthembu kutoka taasisi ya African Field Ranger Training Services ya Afrika Kusini  na Genes Shayo ambaye ni mhifadhi Mkufunzi wa TANAPA

Kikosi hicho Maalum cha TANAPA kilikuwa na askari wapatao 20 ambao walihitimu mafunzo hayo ya askari,lakini mmoja kati ya hao kwa bahati mbaya hakumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya.Aidha kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa askari Mwanamke pekee katika kikosi hicho,aitwaye Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia,amemaliza mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa,alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu kutoka nchini Afrika Kusini na kummwagia sifa za pongezi nyingi kwa uwezo wake kama Mwanamke.
3
Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akirejea kwenye meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
4
Kikosi hicho kikitembea kwa ukakamavu kabisa kusonga mbele tayari kwa kutoa heshima zao kwa wageni rasmi.
6
Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi  akipokea heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi za Taifa,kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa bwa.Adam Swai na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA,Bwa.Martin Loiboki.
10
Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi   akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo ya Uaskari,Frank Anthon Malema,pichani kulai ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA,Bwa.Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo na Mhifadhi wa TANAPA,Bwa.Genes Shayo.

No comments:

Post a Comment