Waziri mdogo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani William Burns yuko mjini Cairo kushinikiza juu ya kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasi baada ya Jeshi kumuondoa madarakani Rais Mohammed Mursi. Burns afisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Marekani kuizuru Misri tangu mapinduzi ya Julai 3, amewasili wakati serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi, ikiimarisha hatua kali dhidi ya wafuasi wa Mursi, huku ikizizuwia mali za maafisa 14 wa ngazi ya juu wa chama cha Udugu wa Kiislamu.
Wakati huo huo viongozi wapya wanaendelea na mpango wa kuunda serikali ya mpito na uchaguzi mpya, lakini wafuasi wa Udugu wa Kiislamu wanashikilia lazima Mursi arejeshwe madarakani.
Jana Mursi alihojiwa na waendesha mashtaka kuhusu malalamiko juu ya makosa kadhaa ya uhalifu.
Wakati huo huo wafanyakazi watatu wa kiwanda kimoja huko Sinai waliuawa katika shambulio la kombora katika eneo hilo linalopakana na Israel.
No comments:
Post a Comment