Wednesday, July 31, 2013

MIKUTANO WA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA NA WANANCHI WA MTAA WA MALIMBE WATOA SULUHISHO KWA KERO ZAO


Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza  ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani (wa pili kutoka kushoto) akisikiliza kero za wananchi wa mtaa wa Malimbe ikiwa ni sehemu ya utaratibu aliouweka kufanya mikutano ya kila mara katika maeneo ya kata yake, wengine katika picha kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa Mtaa Bi Zenaida Musiba, Mtendaji wa kata ya Mkolani Evarist Mtaki, Afisa Ardhi Idara ya Urasimishaji Makazi holela jijila Mwanza Bw. Maduhu Kazi Ilanga, pamoja na Mhandisi wa barabara  halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Malulu.

Mwananchi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Malimbe kata ya Mkolani mkoani Mwanza akitoa hoja ya kuitaka Halmashauri ya jiji iwapatie hati baadhi ya wananchi waliopimiwa viwanja na kufanikisha upimaji wa maeneo ambayo hayajapimwa ili kuwa na uhakika wa makazi yao.

Sehemu ya wananchi wa mtaa wa Malimbe kusanyikoni.

Afisa Ardhi Idara ya Urasimishaji Makazi holela jijila Mwanza Bw. Maduhu Kazi Ilanga, akijibu hoja motomoto za wananchi zilizowasilishwa.

Mhasibu wa Wananchi Mwalimu mstaafu Mzee Mahola aliwasilisha 

Akinamama.

Mwananchi akitoa hoja ya ukarabati wa barabara ya Malimbe - Saut - Mnangani hadi Mkolani Centre ili kupitika kiurahisi. 

Mwananchi huyu alimuomba Mstahiki Meya kuwasiliana na SUMATRA na kuwabana baadhi ya wamiliki wa vyombo vya Usafiri wanaokatiza ruti huku magari yao yakiwa yamesajiliwa kuihudumia njia yote.

Mwalimu Crecency Njogopa aliwakilisha akina mama kwa kulizungumzia suala la uhaba wa maji.

Mdau huyu alimuomba Mstahiki Meya kuwabana Tanesco kuongeza juhudi za kutandaza nguzo za umeme bila urasimu ambapo suala hilo limekuwa kero ya muda mrefu, suala ambalo limechangia kuwaficha wahalifu walioleta maafa ya ujambazi na ubakaji hasa kwa wakazi wapangao maeneo hayo wengi wakiwa ni wanafunzi wa Chuo cha SAUT.

Mhandisi wa barabara wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bw. Malulu akijibu hoja na maswali yaliyojitokeza kwenye mkutano wa wananchi waishio mtaa wa Malimbe. 

Mstahiki Meya akitoa majibu na ufafanuzi kwa yaliyowasilishwa.

Kumalizika kwa mkutano eneo la mtaa wa Malimbe.

Wananchi wakimpongeza Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza mara baada ya mkutano kumalizika huku akitoa majibu mazuri yakitaalamu kupitia safu ya wataalamu alioongozana nao. 

Akina mama nao hawakuwa nyuma kutoa pongezi ambapo ndani yake waliahidi kutoa ushirikiano kwake na wataalamu hao wakati wa utekelezaji.

No comments:

Post a Comment