hebu rejea tamko la mkurugenzi alilotoa mwezi wa saba na kuandika na gazeti lako hili tarehe 14 mwezi wa saba
Mkurugenzi wa manisapaa ya kinondoni ndani ya jiji la Dar es salaam, ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wanoafanya biashara katika maeneo ambayo hayajahalalishwa kukoma mara moja kwa biashara hizo kabla ya kutekelezwa kwa sheria kali.
Tamko hilo la mkurugenzi wa manispaa ya kinondon enginia Mussa Natty ,ameutoa baada ya kutokea kwa matendo kadhaa ya ukaid kutoka kwa wafanya biashara ,wanaofanya kazi zao katika maeneo yasiyo rasmi ,huku wakikaidi agizo la serikali la kuwataka ,kuacha kufanya biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa.
Pamoja na ukaidi huo wa wafanyabiashara katika maeneo yasiyo rasmi,kumetokea sintofaham baada ya wafanyabiashara hao wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara na pengine ndani ya eneo la mradi wa mabasi yaendayo kasi yaani Dat,kufikia hatua ya kuwapiga mawe askari mgambo wa jiji pindi wanapokwenda kuwatoa kwa nguvu.
Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara hao huku akitaja kuwa zoezi kali la kuwakamata wale wote wanaokaidi tamko la kuondoka litaendeshwa na halmashauri ya manispaa ya kinondoni na watakaokamatwa mali zao zitaharibiwa na wahusika kuchukiwa hatua kali.
Akifafanua kuwa zoezi hili la safisha jiji ambalo ameliitaka ni zoezi endelevu amesema litawahusu wale wafanyabisahara wanaopanga vitu pembezoni mwa barabara,waendesha bodaboda wanaopaki katika maeneo yasiyoruhusiwa,wafanyabiashara wakubwa wanaopanga vitu barazani,madereva taxi na wamiliki wa magari mabovu yaliegeshwa pembezoni mwa barabara na maeneo yasiyoruhusiwa.
Hata hivyo mkurugenzi amewataka wafanyabiashara wadogowadogo kuelekeza biashara zao katika magulio na masoko yalioyopangwa kwa ajili yao na kuacha kufanya biashara maeneo yasiyorasmi na kusababisha uchafuzi wa mazingira kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu katika maeneo wanayofanyia biashara kwa sasa.
Baadhi ya meneo ambayo wafanyabiashara wametakiwa kuondoka mara moja ni katika eneo la kituo cha mabasi madogo ya ubongo,kituo cha mabasi madogo mwenge,maeneo yote ya barabara panapoendelea ujenzi wa barabara ya mabais yaendayo kasi au mradi wa Dart unaendelea katika barabara ya morogoro,eneo la Manzese na Tegeta.
Mkurugenzi wa manisaa ya kinondoni enginia Musa ,Amemalizia kwa kusema anawataka wafanyabiashara kuhamisha biashara zao mara moja kutoka katika maeneo yasiyo ruhusiwa na kwenda maeneo elekezi kama soko la makumbusho na soko la mburahati na wale watakao kaidi agizo hili watachukuliwa hatua kali za sheria.
swali linakuja je sheria hizo mbona mpaka leo hazijachukuliwa na mamlaka husika?
|
No comments:
Post a Comment