Wednesday, April 30, 2014

CSSC YATOA MSAADA WA MASHINE YA KISASA YA UPIMAJI MAAMBUKIZI UKIMWI NA UTAFITI YENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 207 KWA HOSPITALI YA SOKOU TOURE MWANZA.



Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akikata utepe kuzindua Mashine ya Kisasa ya kielektroniki yenye jina la kitaalamu Frocytometer ambayo imetolewa kama msaada na Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii Tanzania (CSSC) itumike kwaajili ya utafiti wa maradhi mbalimbali pamoja na upimaji wa viwango vya chembechembe za kinga mwilini (CD4) Gharama halisi ya mashine ni shilingi milioni 207.
Kabla ya uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto yalifanyika maandamano yaliyoanzia viwanja vya vya Nyamagana hadi viwanja vya Hospitali ya mkoa Sekou Toure.
ZIRO - Tokomeza maambukizi mapya ya VVU kwa mtoto.
Waandamanaji waliojitokeza kuchagiza mpango huo.
Wadau toka kada zote wamejitokeza kusapoti mpango huu.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (katikati) akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wakipata ufafanuzi wa Mashine ya Kisasa ya kielektroniki yenye jina la kitaalamu Frocytometer ambayo imetolewa kama msaada na Tume ya Kikristo ya Hudumaza jamii Tanzania (CSSC) itumike kwaajili ya utafiti wa maradhi mbalimbali pamoja na upimaji wa viwango vya chembechembe za kinga mwilini (CD4) Gharama halisi ya mashine ni shilingi milioni 207.
Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Peter Maduki akitoa ufafanuzi.
Emmanuel Lesilwa ni Mtaalamu Mshauri wa Maabara hapa akitoa ufafanuzi juu ya kifaa kinacho beba sample (vipimo) chenye uwezo wa kupima sample 38 ndani ya nusu saa na sample za watu 200 kwa siku. 
Ally Rubisha ni Mtaalamu wa Maabara hapa akichukuwa sample kwaajili ya upimaji.
Baadhi ya akinamama wa jiji la Mwanza (Kushoto na kulia) wakijiandikisha kwa wataalamu wa Afya ili kuingizwa kwenye orodha ya wazazi wanao taka kupima kujua kama ameambukizwa au hajaambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi nia na madhumuni ni kwaajili ya kulinda afya zao na watoto. 
Baadhi ya wakazi wa jiji la mwanza wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kupima maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi, katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa Sekoutoure.
Mmoja kati ya wakazi wa jiji la Mwanza (Kushoto) akipima afya kwa wataalamu wa Afya ili kujua kama ameambukizwa au hajaambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Peter Maduki akizungumza na wananchi walio hudhuria uzinduzi wa kampeni maalumya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto (OPTION B PLUS).
Lega Martin ni mama shuhuda anayeishi na VVU aliyejifungua mtoto asiye na maambukizi hapa anatoa ushuhuda mbele ya ummati ulio fika kwenye uzinduzi wa kampeni maalum ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto. 
Ester Joseph ni mama shuhuda anayeishi na VVU, alibeba ujauzito akiwa na virusi hivyo jeh ni masharti gana, mbinu na njia alizotumia hata akajifungua mtoto salama asiye na maambukizi ya Ukimwi? 
Wadau wasimamizi wa mpango wa ZIRO.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akipiga king'ora kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni maalum ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto.
Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata (mwenye tai katikati) akiwa na wadau wa mradi wa ZIRO wakifuatilia kwa umakini Uzinduzi huo. 
Kwaya uhamasishaji.
Wadau wa Mpango wa ZIRO wakisherehekea uzinduzi

No comments:

Post a Comment