Friday, December 12, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YASHEREHEKEA MAFANIKIO YAKE


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (aliyebeba kombe), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (wa pili kulia), Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Myonge (wa pili kushoto) na viogozi wengine wa Manispaa hiyo wakishangilia na kombe la ushindi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 kitaifa wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Halmashauri hiyo, Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa mmoja wa walimu wakuu wa Shule ya Sekondari Turiani, Beatrice Mhina baada ya shule yake kufanya vizuri katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Halmashauri hiyo, Dar es Salaam juzi. Kushoto kwake ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda, Naibu Meya, Songoro Mnyonge (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Nati.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda kwa kutambua usimamizi wake katika Manispaa hiyo ulioleta mafanikio katika Nyanja mbalimbali wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Mussa Nati.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akikabidhi fedha tasilimu shilingi milioni moja kwa viongozi wa vijana wa hamasa wa Manispaa ya Kiondoni kwa kutambua mchango wao katika kufanikisha ushindi wa kwanza kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014 wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda, Naibu Meya, Songoro Mnyonge (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Nati.
Meya wa Maispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akimpongeza Mama yake msanii nyota wa muziki nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ kwa kutambua mchango wa mwanaye kwa mafanikio yake wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Manispaa hiyo wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.
Wageni waalikwa wakicheza kwaito wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Wenyeviti wa Bodi za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Walimu Wakuu wa shule za Manispaa hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo iliyofanyika Dar es Salaam juzi.

MANISPAA ya Kinondoni imefanikiwa kuvuka malengo ya millennia iliyojiwekea baada ya kupata mafanikio katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo waliohudhuria kwenye hafla ya mafanikio ya Manispaa hiyo, Dar es Salaam juzi Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda aliwataka kuongeza juhudi na kutobweteka na mafanikio hayo kwa lengo la kuboresha maisha ya wakazi wa Manispaa hiyo.

Meya Mwenda alisema kuwa kwa sasa Manispaa yake ina uwezo wa kukarabati miundombinu yake ya usafiri ikiwemo barabara na madaraja kutoka kwenye mfuko wa maafa ma hiyo imetokana na kufanya vizuri kayika ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 8 kwa mwaka 2009 mpaka bilioni 37 kwa mwaka huu.

“Mafanikio haya tunayaenzi na kila mwaka tutahakikisha tunashinda. Nawashukuru watendaji wakiongozwa na Mkurugenzi wao, walimu na wengineo ambao mnaifanya Kinondoni kufikia hapa ilipo.” Alisema Meya huyo.

Mafanikio ya Manispaa hiyo ni pamoja na kuongoza katika mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2014, kuongoza kitaifa mtihani wa kidato cha nne na kutoa wanafunzi 10 bora, ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 8 kwa mwaka 2009 mpaka kufikia bilioni 37 mwaka huu, ongezeko la maabara kutoka vyumba 12 mpaka vyumba 126 na mengine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema Manispaa hiyo imepiga hatua kubwa ukilinganisha na alivyoikuta chini ya usimamizzi wa Meya wake Yusuf Mwenda katika nyanja za ukusanyaji mapato, uwajibikaji na kinidhamu.

Hata hivyo alisema licha ya kutofautiana kimawazo na kimitazamo, lengo ni moja kuona Manispaa hiyo inafikia mahali panapostahili ili kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa bora.

“Kinondoni ya sasa siyo ile niliyoikuta. Imepiga hatua kimapato, uwajibikaji na kinidhamu. Licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo kutofautiana kimawazo na kimitazamo, bado nia yetu ni moja ya kuhakikisha tunaifikisha Manispaa hii pale panapostahili.” Alisema.


Katika hafla hiyo, wadau mbalimbali wakiwemo Walimu Wakuu, Wenyeviti wa Bodi za Shule za Manispaa hiyo, Walipa kodi, Wahandisi na wadau wengine mbalimbali wa maendeleo ya Manispaa hiyo walikabidhiwa vyeti vya kutambua mchango wao katika kuleta mafanikio ya Manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment