Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya tani 78 za sukari ambazo
zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la
Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya
ya Arusha mjini ambao walikuwa
wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari .
Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na
wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25
zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko
1000 kwa ajili ya wananchi wake .
Akiongea na waandishi wa habari kwa
niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician
Mtahengerwa alisema kuwa sukari
sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa
na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa .
Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha
alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani
hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote
ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo
wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa
kwa kufuata utaratibu.
Alisema awali walishagawa sukari tani
45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza
sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa
kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa .
“kunautaratibu wa wafanyabishara
wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa
mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili
sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu
hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata
sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema
Mtahengerwa
Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika
wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri
mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari
litakapo malizika kabisa
Alitoa wito kwa wafanyabiashara
wakubwa ambao wanaingiza sukari kutoa taarifa
katika ofisi husika kwani wakiingiza bila kutoa taarifa iwapo wakibainika watachukuliwa hatua ya kisheria
ikiwa ni pamoja na kutaifishiwa sukari yote
Aidha pia aliwataka wafanya bishara
wadogo wadogo ambao wamepata sukari hiyo kuuza kwakufuata bei elekezi kwani
wanapokiuka agizo hilo iwapo watabainika wameuza kwa bei ya juu tofauti na bei
elekezi sheria kali watachukuliwa ikiwemo ya kuwapeleka mahakamani.
Kwa upande wake mfanyabishara mkuu
ambaye alijitambulisha kwa jina la Romanusi Mwacha alisema kuwa yeye kama mfanyabishara mkubwa ameamua
kumuunga Rais Magufuli mkono kwa kuanza kuuza sukari kwa bei elekezi japo kuwa
amepata hasara kubwa.
Alisema kuwa kama yeye amenunua
sukari shilingi 1900 kilo na bado
ajaweka bei ya usafiri kutoka aliponunua dar adi hapa lakini kutokana na agizo
la serekali ameamua kulifuata na kumuunga magufuli mkono na ndio maana pamoja
yakuwa amenunua bei gali lakini anauza bei raisi kwa kilo shilingi 1700 ili
mfanyabiashara mdogo anaenunua aweze kwenda kumuuzia mlaji bei ya shilingi 1800
kama serekali ilivyoelekeza.
Aliwasihi wafanyabishara wengine
ambao wameficha sukari wazitoe na wale ambao wanauza katika maduka ya reja reja
wauze bei elikezi ili kutoweza kumuumiza mlaji ambaye ni mwananchi .
No comments:
Post a Comment