Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina fupi kuhusu
Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo pichani) inayoendelea mjini Dodoma
chuoni hapa.
Katika
kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya
Umoja wa Mataifa nchini (UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM), mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu
mpango huo na jinsi unavyoweza kubadili maisha yao.
Akizungumza
na MO blog kuhusu mafunzo hayo, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu alisema kuwa mafunzo hayo kwa
wanafunzi wa UDOM ni sehemu wa mafunzo ambayo yanatolewa na ofisi ya UN
nchini ili kuwawezesha Watanzania kuufahamu mpango huo ambao una malengo
ya kubadili maisha ya kila mwananchi, mpango ambao utamalizika mwaka
2030.
Alisema
katika mafunzo hayo wametoa elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya 200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani
wameshatoa mafunzo kama hayo kwa wabunge wa Tanzania lakini pia
wameshafanya mafunzo kama hayo jijini Arusha ambapo yalihudhuriwa na
vijana zaidi ya 200.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa
wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa
semina fupi ilihusisha wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma.
“Tunataka
kila Mtanzania ajue kuhusu Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs)
tumeshatoa elimu sehemu nyingine hii siyo ya kwanza na tutaendelea
kwenda maeneo mengine kutoa elimu zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa
Mataifa nchini ipo imejipanga kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.
Nae
Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof.
Willy Komba alisema mafunzo hayo yamewajenga na kupata elimu ambayo
walikuwa hawajaipata awali inayohusu Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) na pia kueleza kutokana na umuhimu wake watakaa kuangalia ni
jinsi gani wataweka katika mtaala wa masomo ili wanafunzi wajifunze
kuhusu SDGs.
“Sababu
na mimi ndiyo Mkuu wa kitengo cha mitaala nitakaa na wenzangu tuone
jinsi gani tunaweza kuweka katika mitaala yetu ili hata wanafunzi
wajifunze kama masomo, tunawashukuru kwa mafunzo yenu mmetupa changamoto
mpya ambayo hatukuwa nayo,” alisema Komba.
Sehemu
ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakisiliza kwa makini
wakati semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
iliyoendeshwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo
pichani).
Mwanafunzi
wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya habari na
Mawasiliano, Lobezi Kulilo akihoji kuhusiana elimu ya SDGs kuwafikia
watu walio vijijini.
Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta UDOM, Traygod Lyimo akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusiana na SDGs.
Pichani
juu na chini ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipitia
vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za kina kuhusu Malengo 17 mapya ya
Maendeleo Endelevu (SDGs) wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi
ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, akijibu baadhi ya maswali
yaliyoulizwa na wanafunzi wa UDOM wakati wa semina fupi kuhusu Malengo
ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma jana.
Mkuu
wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy
Komba akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia mafunzo
ya SDGs mara baada ya kumalizika semina fupi kwa wanafunzi wa UDOM.
Kutoka
kushoto ni Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), James
Msofe, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye
pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu na Mwanafunzi
wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya Upashanaji
Habari, Lobezi Kulilo katika picha kumbukumbu wakilishilia mabango ya
SDGs.
Baadhi
ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki semina fupi kuhusu SDGs iliyoandaliwa
na ofisi ya Umoja wa Mataifa chuoni hapo katika picha ya pamoja na
vibao vyenye Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wanafunzi wa UDOM mara baada ya kumalizika kwa semina
kuhusu Malengo ya Dunia iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja Mataifa mjini
Dodoma jana.
No comments:
Post a Comment