Wanajeshi wa Marekani wanasema wamewaua wanachama 11 wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda kupitia mashambulio mawili ya kutoka angani karibu na mji wa Idlib nchini Syria mwezi huu.
Miongoni mwa waliouawa ni mshirika mkuu wa zamani wa aliyekuwa kkiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden, wizara ya ulinzi ya Marekani imesema.
Kapteni Jeff Davis, ambaye ni msemaji katika wizara hiyo, amesema wanachama 10 waliuawa kwenye shambulio moja Februari 3.
Shambulio la pili tarehe 4 Februari lilimuua Abu Hani al-Masri, aliyekuwa na ushirika wa karibu sana na Osama Bin Laden.
Al-Masri adnadaiwa kuanzisha na kuendesha kambi za mafunzo za al-Qaeda nchini Afghanistan miaka ya 1980 na 1990
|
Thursday, February 9, 2017
Mshirika wa Osama Bin Laden auawa Syria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment