Bw. Ladislaus Matindi akisamilimiana na Gavana wa Anjoun Mhe. Abdou Salam Abdou
Mazungmzo yakiendelea katika ofisi ya Gavana
Mhe Balozi akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Kisiwa
Mhe Balozi akiongoza kikao na wadau wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun
Mke wa Balozi Mama Irene Kilumanga akimsalim Gavana.
Wajumbe walipowasili Kisiwa cha Anjoun
TAARIFA FUPI ZIARA YA UJUMBE WA ATCL VISIWANI KOMORO TAREHE 06 FEBRUARI, 2017
Ujumbe wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL Limited) uliwasili Visiwani Komoro tarehe 5 February, 2017. Ujumbe huo ukiongozwa na Bw. Emmanuel Korosso ulipokelewa na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, Visiwani Komoro. Aidha Mwenyekiti huyo aliongozana pia na Bw. Ladislaus E. Matindi Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL.
Madhumini ya ziara hiyo ilikuwa ni kuja kuangalia namna gani ATCL inaweza kutanua wigo wa safari zake Visiwani Komoro. Hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo kuweza kulidhibiti kikamilifu soko la anga la Visiwa vya Komoro ambapo kwa sasa Soko hilo limekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika mengine ya Kimataifa kama vile Ethiopian Airlines, Air Madagscar, Kenya Airways n.k.
Katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kuongozana na Mhe. Balozi kwenda Kisiwa cha Anjoun na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe. Abdou Salami Abdou. Ifahamike kwamba Shirika la ndege la ATCL hufanya safari zake mara tatu kwa wiki Visiwani Komoro ambapo ndege hiyo hutua katika uwanja wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim Jijini Moroni.
Komoro ni Muungano wa Visiwa Vitatu ambavyo ni Anjoun, Ngazidja na Moheli. Hata hivyo imeonekana kuwa abiria wengi wanaosafiri kuja Tanzania kwa ajili ya shughuli za biashara hutokea Katika Kisiwa cha Anjoun. Imejidhihirisha kuwa abiria kutoka Ksiwa cha Anjoun hupata usumbufu kwa vile hakuna safari za moja kwa moja kutoka Kisiwa hicho kwenda Dar es Salaam, hali ambayo imeonekana kuongeza ghara za usafiri kwa abiria hao.
Aidha katika mazungumzo yao na Gavana wa Kisiwa cha Anjoun ujumbe huo uliwasilisha maombi ya ATCL kupewa kibali cha kutua Kisiwa cha Anjoun ambapo Gavana huyo aliridhia maombi hayo na kueleza kufurahishwa kwake na dhamira ya ATCL kufanya safari zake Kisiwani hapo.
Mhe. Gavana alieleza pia safari za ATCL Visiwani hapo zitasaidia katika kukuza mahusiano ya biashara kati ya Tanzania na Komoro pamoja na kupunguza gharama za usafiri kwa abiria wanaotokea kwenye Kisiwa hicho. Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro, Mhe. Chabaka Kilumanga alieleza pia kuwa jukumu kubwa la Ubalozi ni kuhakikisha kuwa mahusiano ya biashara kati ya Tanzania yanakuzwa na kwamba usafiri wa anga ni njia moja wapo ya kukuza mahusiano hayo. Mhe. Balozi aliendelea kwa kueleza kuwa lengo ni kuona Dar es Salaam inakuwa ni kitovu cha Biashara hivyo hakuna budi kukawepo ufanisi katika usafiri wa anga na usafiri wa maji.
Sambamba na hilo, Ujumbe wa ATCL pamoja na Balozi walipata fursa pia ya kufanya mazungumzo na wadau kutoka Sekta ya Biashara wa Kisiwa cha Anjoun ambapo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Ladislaus Matindi aliwahakikishia wana Anjouna kuwa shirika la Ndege la ATCL la sasa sio kama la zamani na kwamba shirika hilo limejidhatiti katika kuboresha huduma zake.
Aidha Mkurugenzi huyo alieleza kuwa shirika hilo limeweza kuondoa usumbufu mwingi uliokuwa ukijitokeza hapo nyuma ikiwemo suala la upotevu wa mizigo, kufutwa kwa safari bila maelezo, ucheleweshaji wa abiria na mizigo yao, alieleza kuwa shirika hilo linatambua umuhimu wa wadua wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun na ndio maana ameeongozana na Mwenyekiti wa Bodi Visiwani hapa ili kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanya biashara hao na kushauriana juu ya namna gani changamoto hizo zitapatiwa ufumbuzi.
Kw upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL Bw. Emmanuel Korosso alielekeza shukurani zange kwa wadau wa biashara Kisiwani Anjoun na kuendelea kusisitiza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limedhamiria katika kuboresha ufanisi kwenye utendaji wake na kwamba shirika hilo linasimama pamoja na Wakomoro katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa.
Mwenyekiti aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili abiria wa Anjoun na kwamba changamoto hizo siku zake zinahesabika. Aliahidi kuwa yale yote ambayo ATCL imedhamiria kufanya yatatekelezwa tena kwa wakati muafaka kwani Ofisi ya Ubalozi ipo kwa ajili ya kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment