Monday, April 30, 2012

Huku tuendako ni pabaya zaidi

marehemu Mussa MBWAMBO enzi za uahai wake

hakika ni tukio la kusikitisha sana kati ya matukio yaliyo wahi kutokea katika jiji la A rusha na  vitongoji vyake ,si tukio lingine ila ni tukio lililochukua uhai wa kamanda wa chadema bwana Mussa Mbwabo


alikuwa ni Mwenyekiti wa kata ya Usa River mkoani Arusha wa Chadema, na tukio la kifo chake lilitokea pale watu wasio julikana walipoamua kuutoa uhai wake kwa kumchinja bila huruma na kutoa uhai wake

Taarifa za tukio hilo la kikatili zimetolewa na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nasari wakati akizungumza na moja kwa moja na kituo cha Radio cha Sunrise radio Arusha toka eneo la tukio.

Nasari amesema kuwa wao kama wana chadema na wakazi wa Usa River wanaliomba  jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kubaini chanzo cha tukio hilo.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema  kuwa kabla ya tukio hilo marehemu Mbwambo alikuwa na wenzake kwenye eneo la starehe huku akinywa soda ,na wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake  ghafla alipigiwa simu na watu ambao hakuwafahamu wakimuambia  kuwa kulikuwa na wanachama wa ccm wanataka kurudisha kadi na kujiunga na Chadema basi marehemu aliamu kwenda kuwafuata watu hao kutokana na maelekezo waliyompa kwenye simu .

lakini hakurudi tena nnyumbani kwake  hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa kandokando ya barabara eneo la makaburi,huku pikipiki na vitu vingine alivyokuwa navyo isipokuwa simu yake  vikibaki eneo   hilo bila kuchukuliwa na wauaji hao.


                                  
huwezi amini ila ukweli ndio huu,huu ndio mwili wa marehemu Musa baadaya ya mauaji

hakika ni mauaji ya aina yake blog hii inawapa pole wafiwa wote na wale wote walioguswa na msiba wa Musa Mbwambo mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepni .

kwa wale wenye nafasi kesho 01 /5/ wafike usa kwa mazishi ya marehemu Musa

No comments:

Post a Comment