Thursday, April 26, 2012

mwenye nacho huongezewa na asienacho hunyangaywa kabisaaa ......?

mkazi mmoja  wa Mwenge Dar es Salaam   HOYCE Lyimo,, amelalamika kuvadhulumiwa  eneo lake na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chakechake (CUF), Fatma Maghimbi, ambaye amerejea CCM.Lyimo anadai alinunua shamba hilo lililopo maeneo ya Mwenge, Lufungira na mume wake mwaka 1978 kutoka kwa Roman Mrema.

Mwaka 2010, Maghimbi alimfungulia kesi Lyimo katika Mahakama Kuu akidai ndiye mmiliki halali wa eneo hilo. Hata hivyo, hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa Agosti mwaka jana, ilimtaja Maghimbi kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.

Kutokana na mwenendo wa kesi hiyo, mwanamke anadai Maghimbi alitumia fedha kupata ushindi.
“Baada ya hukumu hiyo kutolewa niliamua kukata rufaa, lakini nilipompelekea barua ya kuitwa mahakamani, Maghimbi alijificha ndani,” alidai Lyimo na kuongeza:
“Watu wamemwona, lakini kila mjumbe alipopeleka barua hiyo aliambiwa hayupo.”
Lyimo anadai alijitahidi kwenda nyumbani kwa Maghimbi zaidi ya mara nne bila mafanikio akielezwa kuwa ametoka.

Siku mbili baada ya kujaribu kumfikishia barua hiyo bila mafanikio, kundi la ‘mabaunsa’ lilifika bila taarifa yoyote na kuanza kuvunja vibanda va maduka vilivyopo eneo hilo na kuharibu mali zote zilizokuwamo.

“Hata kama hukumu ilikwishatolewa, lakini mimi nilikata rufaa na nimepeleka barua ya mahakama nyumbani kwake, iweje avunje bila hata kunipa taarifa?” anahoji Lyimo..
Lyimo ambaye mume wake, Deus Mtei, alifariki mwaka 1996 alionyesha nakala zote za mauzo ya kiwanja hicho kutoka Mrema mwaka 1978.

Akizungumzia tuhuma hizo, Maghimbi alisema aliponunua eneo hilo alimwachia mwanamke huyo kwa muda ili aendeleze vitega uchumi ambavyo ni vibanda vya maduka na kilimo cha mbogamboga.

“Yeye ni mkristo, haoni kuwa anafanya dhambi ya kuiba, aliniomba alitumie eneo lile kwa muda, sikuwa na hiyana nikamwachia leo hii anigeuke kuwa ni lake?” alihoji Maghimbi.

Maghimbi alisema hata viongozi wa serikali za mitaa wanafahamu eneo lile ni la kwake na walitoa ushahidi mahakamani.

Pia, alisema Mahakama ndiyo inayosema ukweli, lakini siyo malalamikaji wala  yeye (Maghimbi).
“Mahakama imekwishaamua kuwa mimi ndiye mmiliki, kipi cha zaidi … kwa kuwa amekata rufaa, tusubiri tena hukumu,” alisema Maghimbi na kuongeza:

 “Mimi ninafahamu sheria, wala sitetereshwi, kama kiwanja ni changu, basi atafidia gharama zote, ikiwamo za mahakama na usumbufu na iwapo mahakama itasema ni chake, basi nitamlipa gharama za usumbufu na fremu zake.”

Mrema alisema alimuuzia kiwanja Lyimo mwaka 1978, alimpimia kiwanja hicho na kuwauzia kwa malipo ya Sh500.

“Ninaufahamu ukubwa wa kiwanja hadi mpaka wake, niliwauzia mimi mwenyewe, Maghimbi amekuja hapa juzi, kwa nini anyang’anye haki ya watu?” alihoji Mrema.

Mrema alisema Maghimbi alipojenga nyumba hiyo mwaka 2004, alijenga ukuta kuzunguka eneo lake, lakini mwaka 2010 alianza kudai kuwa eneo la Lyimo ni la kwake

“Mwenye kisu kikali amekitumia kula nyama, mdhaifu asiye na kisu amekosa haki yake, tutafanyaje?” Mrema alimaliza kwa kuhoji. 



haya wanaharakati kazi ni kwenu mteteeni mama huyu

No comments:

Post a Comment