Monday, June 25, 2012

Idadi ya waliouwawa shambulio la Mombasa yaongezeka

Idadi ya waliouwawa katika shambulio la guruneti kwenye baa moja mjini Mombasa jana, sasa imeongezeka hadi watu watatu.
Shambulio hilo ni pigo jengine kwa serikali ya Kenya katika juhudi za kuifufuwa sekta ya utalii.

 Mtu mmoja alikufa papo hapo mahala pa shambulio na wengine wawili wakafariki hospitali.Inashukiwa huenda  shambulio hilo limefanywa na waasi wa Kiislamu wa Al-shabaab kutoka Somalia na limefanyika baada ya Marekani kuonya raia wake wanaokwenda Mombasa, ikisema imepokea taarifa ya uwezekano wa shambulio la kigaidi mjini humo.


 Guruneti hilo liliripuka katika baa moja  kwenye wilaya ya Mishomoroni, ambako umati mkubwa wa wapenzi wa kandanda walikuwa wakiandalia pambano la  robo fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya kati ya England na Italia.    

No comments:

Post a Comment