Monday, June 25, 2012

Baraza la mawaziri Kuwait lajiuzulu

Baraza la mawaziri  nchini Kuwait limejiuzulu. Kujiuzulu huko leo kumekuja siku kadhaa  baada ya mahakama kuu kubatilisha uchaguzi wa bunge.

Kituo kimoja cha binafsi cha televisheni Al-Rai, Kimesema  kwamba baraza hilo la mawaziri liliwasilisha hati ya kujiuzulu kwa Mfalme wa nchi hiyo, lakini hapakutolewa taarifa zaidi.


Baraza hilo liliundwa miezi minne tu baada ya uchaguzi wa bunge mwezi Februari mwaka huu, ambapo upinzani ulipata ushindi mkubwa na wingi wa viti bungeni.

Lilikuwa ni baraza la mawaziri la  tisa katika Falme hiyo yenye utajiri wa mafuta tokea Februari 2006
. Mawaziri wawili katika baraza hilo lililokuwa na mawaziri 16, walilazimika kujiuzulu wiki chache zilizopita, baada ya kushinikizwa na wabunge.

No comments:

Post a Comment