Saturday, May 17, 2014

UN:Ukiukaji wa haki za binadamu Ukrain


Umoja wa Mataifa umetoa ripoti hiyo huku Ukraine ikiwa bado katika mzozo wa kisiasa

Ripoti mpya iliyotayarishwa na wachunguzi wa umoja wa mataifa kuhusu visa vya ukiukaji wa haki za binadamu inasema haki za binadamu nchini Ukraine zimezorota kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maandamano ya amani kwa wakati mwingi yanageuka na kuwa vurugu, waandishi wa habari pamoja na wachunguzi wa kimataifa wanakamatwa na kuzuiliwa huku wapinzani wakiuwawa.
Ripoti hiyo inasema ukiukaji wa sheria umekithiri maeneo ya Mashariki na Kusini na kumekuwa na visa vya watu kulengwa katika njama za mauaji, kuteswa na kutekwa nyara.
Uhalifu huu unatekelezwa na vikosi vinavyoipinga serikali mashariuki mwa Ukraine. Urusi inasema kuwa ripoti hiyo inaegemea upande mmoja na imejaa mapungufu makubwa.

No comments:

Post a Comment