Monday, June 25, 2012

Umoja wa Ulaya waiwekea vikwazo vipya Syria


Umoja wa Ulaya umeiwekea Syria vikwazo vipya leo vinavyolenga wizara sita, benki pamoja na kituo cha televisheni.
 Vikwazo hivyo vipya ni vya 16 kuwekwa na umoja huo tangu kuanza kwa vuguvugu la kuupinga utawala wa Rais Bashar al- Assad mwezi Machi mwaka jana.

Hatua hiyo ambayo imepitishwa na Mawaziri wa Kigeni wa nchi mwanachama wa umoja huo leo, imeongeza idadi ya watu waliopigwa marufuku kuingia nchi za ulaya kufikia 129 pamoja na mambo mengine kwenye vikwazo kuwa 49.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza William Hague amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu ili kurekebisha hali ilivyo nchini Syria.
 Naye Mkuu wa Sera za Kigeni wa umoja huo Catherine Ashton amesema kuwa kadri utawala wa Assad utakavyoendelea kuwakandamiza watu ndivyo vikwazo vitakavyoongezeka.

No comments:

Post a Comment