Monday, June 25, 2012

WAONYWA KUTUMIA BARUTI

WIZARA ya Nishati na  Madini hususan Ofisi ya madini kanda ya kaskazini wamekea  vikali wachimbaji wa madini ambao wamekuwa wakitumia baruti kama silaha mbadala ya kuzitumia kama nyenzo za kazi ya  uchimbaji.

Akizungumza na wandishi wa habari kamishna wa madini kanda ya kaskazini Mhandisi Benjamini Mchwampaka amesema kuwa vitendo hivyo viovu vinatokana na wachimbaji wa wasiokuwa na maadili ya uchimbaji madini ambao wanatumia baruti kutengeneza mabomu ya kienyeji na kuwatupia wachimbaji wa migodi ya jirani.

Mhandishi Mchwampaka ameongeza kuwa ofisi yake haitolifumbia macho suala hilo kwa kuwa huo sio uchimbaji bali ni uhalifu kwa kuwa una lengo la kuwaumiza na kuwatisha kusudi wawafukuze ili kuchukua maeneo yao ambayo yanahisiwa kuwa na uzalishaji wa madini.

Aidha ametaja maeneo ambayo  vitendo hivyo vimeshamiri sana kwenye migodi inayopakana na moigodi ya Kampuni ya Tanzanite One kwenye kitalu C.

Amefafanua kuwa mgodi wowote ambao utabainika kwamba wachimbaji wake wanajihusisha na vitendo vya kuwatupia mabomu wachimbaji wa migodi jirani,mgodi huo utafungwa mara moja na leseni husika itafutwa na wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia amewataka Mameneja  na wachimbaji kuwa ni lazima kutangaziana  baruti ama moto kabla ya ulipuaji baruti kufanyika  ili kuthibiti vitendo viovu.

No comments:

Post a Comment