Fabrice Muamba aonyesha dalili za kuimarika
Klabu ya Bolton Wanderers imesema kiungo wake anayeugua Fabrice
Muamba sasa anaweza kupumua mwenyewe lakini angali katika hali mbaya.
Muamba yuko katika hospitali ya London Chest nchini Uingereza.
Katika taarifa ya pili kutoka kwa klabu hiyo ya ligi kuu ya soka
Uingereza, ni kuwa Muamba anaendelea kuonyesha dalili za kuimarika, siku
mbili tu baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo wakati wa mchuano wao wa
kombe la FA. Taarofa hiyo ilisema sasa anaweza kupumua kwa kujitegemea
bila usaidizi wa mitambo. Pia anaweza kuwatambua watu wa familia yake na
kuyajibu maswali ipasavyo.Huku hayo yakijiri, mchuano wa ligi ya Uingereza kati ya Bolton Wanderers nyumbani kwa Aston Villa uliotarajiwa kuchezwa kesho umeahirishwa kutokana na hali ya Muamba. Maafisa wa ligi wamesema mchuano huo umeahirishwa kutokana na ombi la klabu ya Bolton. Wachezaji wa Bolton hawako tayari kucheza mchuano huo na hivyo utapangwa tena baadaye. Mchuano utakaofuata utakuwa dhidi ya Blackburn Rovers siku ya Jumamosi.
Dortmund na Bayern wapepea
Katika ligi ya soka Ujerumani – Bundesliga, mabingwa Borussia Dortmund waliendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi tano baada ya ushindi wao wa goli moja bila jawabu mwishoni mwa wiki dhidi ya Werder Bremen.
Wakati huo huo Bayern Munich na Borussia Dortmund wataendeleza vita vya ubabe wao katika soka ya nyumbani kuwania kombe la shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal wakilenga kukutana katika fainali. Mabingwa wa ligi na ambao ni viongozi Dortmund watasafiri kuchuana na klabu ya daraja la pili Greuther Fuerth katika nusu fainali ya kwanza kesho Jumanne. Kisha Jumatano mabingwa watetezi wa taji hilo Bayern Munich watakuwa nyumbani kwa mahasimu wao wa Bundesliga Borussia Moenchengladbach katika nusu fainali ya pili. Fainali itakuwa Mei 7 katika uwanja wa Olimpiki jijini Berlin.
Saudi Arabia kuwatuma wanawake katika Olimpiki
IOC imesema leo kuwa maafisa wa Kamati ya Olimpiki ya Saudi Arabia wamewasilisha orodha ya wanariadha wa kike wanaoweza kushiriki mashindano hayo ya Olimpiki jijini London.
Shirika la haki za binaadamu la Humans Rights Watch liliwashutumu waandalizi wa michezo ya Olimpiki kwa kile lilichokitaja kuwa ni ubaguzi wa kijinsia kutoka mataifa ya Ghuba ya Kiarabu ya Saudi Arabia na Qatar, pamoja na nchi ndogo ya Kusini Mashariki mwa Asia Brunei. Qatar inayowania fursa ya kuandaa mashindano ya Olimpiki mwaka 2020, ilisema itawatuma wanariadha wanawake katika mashindano ya Olimpiki London kwa mara ya kwanza.
Bayern mguu mmoja katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa
Miamba ya Bundesliga Bayern Munich waliiweka hai ndoto ya
kucheza fainali ya ligi ya Mabingwa katika mji wao wa nyumbani. Hii ni
baada ya kushinda mchuano wa mkondo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya
Olympique Marseille
Magoli katika kila kipindi kutoka kwa Mario Gomez na Arjen Robben
yaliipa Bayern Munich ushindi wa mabao mawili kwa sifuri nyumbani kwa
Olympique Marseille Jana Jumatano. Ushindi huo umewaweka miamba hao wa
ligi ya soka Ujerumani – Bundesliga hatua moja karibu na nusu fainali ya
kombe la Mabingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.Wakati huo huo, mabingwa wa ulaya Barcelona walitoka sare ya bila kufungana na viongozi wa ligi ya soka Italia Serie A AC Milan uwanjani San Siro na kuwacha nafasi ya robo fainali kusalia wazi.
Ushindi wa Bayern unawafanya kuwa timu bora inayopigiwa upatu kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Real Madrid ambao siku ya Jumanne walishinda magoli matatu wka sifuri nyumbani kwa APOEL Nicosia katika mechi y amkondo wa kwanza.
Bayern iliumiliki mpira
Lakini Bayern walijipa bao la pili la afueni wakati Robben alipocheza gonga nipe gonga nikupe na mwenzake Thomas Mueller kabla ya kuweka wavuni bao safi lililombwaga kipa Andrade. Kisha vijana hao wa kocha Jupp Heynckes wakachukua udhibiti kuanzia hapo hadi mwisho.
Schweinsteiger kukosa mchuano wa marudiano
Akizungumza baada ya mchuano kocha Heynckes alisema kitu cha pekee ambacho hakikuwa kizuri kwao ni kwamba walipata kadi za njano. Moja ilimwendea mchezaji wa akiba Bastian Schweinsteiger ambaye sasa hatacheza katika mchuano wa marudiano. Naye Robben alisema wangali na mchuano mmoja wa kucheza nyumbani Allianz Arena. Aliongeza kuwa mchezo wao ulikuwa mzuri pamoja na matokeo na sasa kuna uwezekano wa wao kukutana na Real Madrid katika nusu fainali.
Mario Gomez sasa anapungukiwa goli moja tu nyuma ya Lionel Messi aliyedhibitiwa vikali na AC Milan katika mchuano mkali ulioishia sare ya bila kufungana mjini Milan uwanjani San Siro, mchuano ambao pande zote mbili zilikuwa na nafasi nzuri za kufunga lakini hazikuzitumia vyema.
Barcelona watokwa jasho Milan
Barcelona waliumiliki mpira kw akiwango kikubwa lakini walikuwa na matatizo ya kufanya mashambulizi yoyote katika lango la adui Milan ambao walikuwa wamejpanga vyema katika safu yake ya ulinzi, hadi dakika za mwisho wakati vijana hao wa kocha Pep Guardiola walipokaribia mara mbili kupata bao.
Carles Puyol alipiga kichwa juu ya lango kutoka mkwaju wa konakatika dakikay a78 nao mkwaju wa Messi ukaokolewa langoni na kipa wa Milan Christian Abiatti, dakika mbili mchuano kukamilika, huku naye Cristian Tello akasukuma shuti lililozuiwa.
Barcelona kuamua Camp Nou
Messi ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufunga magoli matano katika mchuano mmoja wa ligi ya mabingwa, wakati Barca ikiwazaba Bayer Leverkusen 7 – 1 katika awamu iliyopita, angali anahitaji goli la 50 la taaluma yake katika kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa. Lakini vijana hao wa Pep Guardiola wana fursa ya kufanya vyema katika mkondo wa pili uwanjani Camp Nou Jumanne ijayo. Mshindi atakutana na Chelsea au Benfica katika nusu fainali, huku klabu hiyo ya Premier League ikiongoza kufuatia ushindi wao wa moja sifuri mjini Lisbon siku ya Jumanne.
Kipa wa Barca Victor Valdes amesema walikuwa na nafasi nyingi lakini hawakuzitumia vyema. Kwamba walijaribu kupokezana pasi fupi wakati wakiumiliki mpira kwa muda mrefu. Anasema mchuano bado ni wazi na sas autaamuliwa uwanjani mwao.
No comments:
Post a Comment