Tuesday, March 6, 2012

Wanafunzi wa THE ARUSHA EAST AFRICA TRAINING INSTITUTE watembelea redio ya jamii ya ORKONEREI REDIO SERVICE (ORS)mkoani Manyara

Tareh 2 mwezi march mwaka 2012 itakuwa histori kwa wanfunzi wa EATI baada ya kwenda kujifunza kwa kujionea vile mabyo huwa wanajifunza kila wakati pale wanapokuwa darasani .
Safari hiyo ya kimasomo ambayo iliandaliwa na chou chini ya uongozi wa wanafunzi ulishirikisha wanafunzi 14 wa ngazi mbali mbali kuanzia cheti mpaka stashahada kwa wale ambao wanasomea uhandishi wa habari.
Mwalimu Abuabakari aliongoza msafara huo kwa niaba ya ya uongozi wa cho amabapo kwa upande wa wanafunzi Gasper ambaye ni rais wa chuo aliamabtana na wanachuo akisaidiwa na joseph amkani ambaye ni kiongozi wa mambo yote ya jamii na burudani.
Wakiwa huko manyara wanchuo hao walipata fursa ya kutembelea kituo cha redio Kama wanavyoonekana hapo chin Cha ajabu hii redio ya taasisis inamtambo mkubwa yaani transimiter kubwa na inachuka nafasi ya pili ikitanguliwa na ile ya TBC picha inajionyesha hapo chini
Wanachuo pia walipata fursa ya kutembele chumba cha uzalishaji yaani production studio na huko mengi yalifanyika Hawakuishia hapo kwani pia walipata fursa ya kufanya kipindi live kipindi amacho kilirushwa hewani kiitwacho kijana na jamii Kama si haba wanachuo pia walipata fursa ya kucheza mechi ya kirafiki na wanhabari wa ors ambapo matokea yalionyesha timu zote kutoka suluhu tatu kwa tatu.na kufutiwa na musiki wa kukatwa na shoka ambao ulirushwa na madj wakali ambao ni DJ ID OLE MAIKA,DJ THE TRONG JOSEPH AMANI na DJ SIR MBWETI
Kama haitoshi wanafunzi hao pia walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kusindika maziwa cha ENGITENG na huko walijifunza mengi .
KWA HAKIKA TUNAWASHUKURU SANA UONGOZI WA ORS DADA HADIJA,MR BARAKA,KIWALE,JUDITH SHANGO ,DADA SCOLA na wengine wote kwa kweli ukarimu wenu ni wakuigwa na media zote hapa nchini .

No comments:

Post a Comment