Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii
Mama mmoja alijikuta akianguka na kukosa nguvu ghafla kufuatia uchungu mkubwa wa kifo cha mpendwa wao Steven kanumba.
Hongereni
sasa wafanyakazi wa chama cha Msalaba Mwekundu,kwa hiki mlichokifanya
hapa lidaz Club,Mungu awape nguvu,imani na upendo kwa wakati huu mgumu
tulionao sasa.
Wa
Pili kulia ni Mama yake na Marehemu Steven Kanumba akiwa ameambatana
ndugu jamaa na marafiki kumuaga mtoto wao kabla ya kwenda kulazwa kwenye
nyumba yake ya milele jioni ya leo.
Kikundi cha kwaya kikiimba mbele ya umati mkubwa wa watu uliofika kwenye viwanja hivi kumuaga mpendwa wao.
Umati wa watu uliojitokeza Kuaga
mwili wa marehemu steven Kanumba katika viwanja vya Leaders Club
jijini Dar es Salaam, sasa watu ni wengi hadi imeshindikana kuaaga
jambo ambalo limepelekea watu kuzimia hovyo hasa akina dada,huku
kikubdi cha huduma ya kwanza kutoka Red Cross kikifanya kazi yake
ipasavyo kuwasaidia watu mbalimbali waliokuwa wakikubwa na tatizo la
aina yoyote.
Rais
wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini,Saimon Mwakifwamba akisoma
hotuba fupi iliyohusu mambo mbalimbali kuhusiana na msiba huo mkubwa wa
kuondokewa na Mpendwa wetu,Steven Kanumba.
Wapigaji wenzangu nao wako bize kuchukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu.
Watu wengi walizimia kama uonavyo pichani,hasa wanawake ambao kiukweli walikuwa na hisia sana juu ya msiba huu.
Utaratibu ukiwekwa sawa kwa ajili ya kumuaga marehemu Steven kanumba.
Gari iliyokuwa imebeba mwili wa Marehemu Steven Kanumba ukiwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club leo asubuhi tayari kwa kuagwa.
Umati mkubwa wa watu ukiwa nje ya viwanja vya lidaz mapema leo asubuhi wakati wa kuaga mwili wa marehemu,Steven kanumba.
No comments:
Post a Comment