Bongo
movie ndio taito ya filamu za Kitanzania ambapo umaarufu wake
umechangiwa sana na Ndugu Steven Charles Kanumba ambaye kwa sasa ni
marehemu, Sanaa hiyo ya filamu na maigizo hapa Tanzania na hata afrika
imepta pigo ambalo halitasahaulika kwani imeondokewa na kijana mdogo
ambaye mchango wake hata nusu yake haujafikia. Taarifa za kuaminika
kutoka kwa ndugu, jmaa na marafiki wa karibu wa msanii huyo zinadai kuwa
kifo chake kilitokana na
Polisi
mkoani Dar es Salaam imethibitisha kuwa inamshikilia kwa mahojiano
msanii huyo wa kike kutokana na kuhusika na kifo cha Kanumba, ambaye
alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na
hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi
ya wasanii Maarufu wa Kinigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika Michezo ya luninga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama Bongo Movies. Taratibu za msiba zinaendelea nyumbani kwake Sinza Vaticany.
















No comments:
Post a Comment