''Hata
tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani katika tasnia ni kazi
bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na sivinginevyo kama
wanichukia moyoni basi onesha usoni na kama wanipenda moyoni basi onesha
usoni na si vinginevyo,Isiwe moyoni wanichukia alafu usoni
wanichekea,Hii sanaa ni karama tuliyobarikiwa na Mungu tuitumie vyema
kwa ajili ya utukufu wake maana ipo siku atatuuliza na kutudai,kama
katupa bure basi anao uwezo wa kutuny'ang'anya pia'' soma Wakorintho
uone jinsi Mungu alivyogawa karama hizi na ni kwanini katugawia.
Haya si maneno yangu bali ni yake Marehemu Steven Kanumba ambayo aliyasema wakati wa Tuzo za ZIFF kule Zanzibar.
Bila
shaka hii leo wakati tunaenda Kupokea Ufufuo wa Bawana wetu Yesu Kristo
hiyo kesho (Pasaka) Kanumba kama atapata nafasi ya kuhojiwa huko aliko
hii leo juu ya Karama ya uimbaji na uigizaji aliyopewa aliitumia vipi
basi jibu Alisha tuachia na hakika usoni alituonesha dhahiri kuwa
uigizaji anauweza na kipaji anacho sijui katika matendo yake ya
kumpendeza Mungu moyoni.
Wengi
wamekufa, katika tasnia ya Filamu na maigizo hapa nchini, lakini kifo
cha Steven Kanumba "The Great Pioneer" kinasemwa kuwa ni kifo kilicho
leta kishindo na mshtuko mkubwa sana miongoni mwa wasanii na wapenzi wa
filamu hapa nchini.
Mitandao
mingi ya kijamii imetapakaa habari mbalimbali juu ya Kifo cha Msanii wa
Magizo na filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba.
Steven Charles Kanumba (28) ndio jina lakehalisi akiwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia ya Bwana na Bibi, Charles Meshak Kanumba.
Kanumba alizaliwa yeye na dada zake wa wili huku yeye akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia hiyo.
Alizaliwa
januari 8, 1984, akiwa ni Msukuma kutoka mkoani Shinyanga alipata elimu
yake ya Msingi katika shule ya Msingi Bugoyi mkoani humo.
Alipo
maliza elimu yake ya Msingi Kanumba alijiunga na elimu ya Sekondari
katika shule ya Mwadui seminari na baade alipofika kidato cha pili
kuhamia katika Shule ya Christian a Seminari iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Alihitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi .
Kanumba
aliwahi simulia kuwa uigizaji ni kitu ambacho kipo katika damu yake na
alikuwa akikipenda na kutamani kuwa mwigizaji tangu akiwa mdogo. Alianza
uigizaji akiwa mdogo kwa kufanya maigizo Kanisani.
Mbali na Uigizaji Kanumba pia alipenda sana kuimba na alifanya hivyo akiwa kanisani na shuleni.
Baada
ya kuambiwa na watu kuwa anakipaji cha kuigiza ndipo Marehemu Kanumba
alipoamua kujiunga na kundi la Kaole ambalo lilikuwa na waigizaji
wakongwe ambao hivi sasa baadhi yao wamefariki kama akina mzee Kipara,
Pwagu na wengine waliopo kama akina Bui Mwenda, Mashaka na wengine
wengi.
Kanumba akiwa katika kundi hilo mbali ya kukutana na wasanii hao wakomngwe ambao alijifunza mengi lakini pia alipata kufundishwa akiwa hapo na walimu kadhaa kutoka chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Kanumba
baada ya kukaa kwa takribani mwaka mmjoa akijinoa na Kaole sanaa Group
alipata mafunzo pia ya uigizaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
chini ya usimamizi wa Dkt Nyoni ambaye alimfunza kwa miezi 3.
Hakika
ni kipaji chake cha uigizaji mahiri na kuipenda kazi yake ndivyo
viliweza kumjengea jina marehemu Kanumba na hatimaye kuweza kuanza
kuteka hisia za watu na mashabiki.
Kanumba alijizolea Sifa nyingi sana ambazo kwa kiasi kikubwa zimemletea mafanikio katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kanumba
baada ya mafanikio hayo katika uigizaji alimua kupiga hatua mbele na
kuingia katika ulingo wa utengezaji wa filamu hapa nchini.
Katika
filamu napo Kanumba amefanya fyema na kutamba vilivyo katika ualimwengu
huu wa Filamu za Bongo “ Bongo Movie” na kulishika vilivyo soko hilo la
filamu hapa nchini.
Kanumba aambaye ametutoka ghafla kwa maana ya bila kuugua na kifo chake kustua wengi hasa katika mapenzi yao makubwa katika filamu zake wataendelea kumkumbuka katika filamu zake kali za kusismua na mafunzo lukuki za Kiswahili.
Miongoni na Big Dady, Because of You, Devel Kingdom, Moses, This is It, More Than Pain, Off Side, Uncle JJ, The Shock, Young Billionaire na Description filamu iliyopo sokoni hivi sasa ni Kijiji cha Tambua HAKI na hivi karibuni alikuwa njiani kuzindua filamu yake mpya ya Ndoa Yangu.
Ni
filamu ambazo hizi ambazo ziliweza kumzungusha Kanumba katika nchi
mbalimbali duniani kama Nigeria, Ghana, Amerika na ulaya katika ama
kurekodi filamu hizo au kukutana na watu mbalimbali wa tasnia yake na
kujifunza mengi.
Zipo Filamu kati ya hizi ambazo ameigiza na waigizaji kadhaa kutoka Nigeria na Ghana.
Kanumba alipata mwaliko wa kushiriki katika tamasha kubnwa la Filamu la Nchini Ghana ambalo linajulikana kamam Festival of Films in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.
Hapa
nchini Kanumba atakumbukwa sana na wacheza filamu na wazalishaji kama
yeye ambao katika uhai wake aliwahi kufanya nao kazi kama vile Pitchou
Mwamba, Ray, Aunt Ezekiel, JB, Wolper, Irine Uwoya, Aunt Ezekiel, Lulu,
Jenifer, Patrick, Sofia, Rich Rich, na wengineo kibao.
Nje
yamipaka ya Tanzania kanumba amewahi kuigiza filamu zake hizo na
wasanii Nollywood kule Nigeria na alipata pia kutembelea ngome ya
Hollywood, Warner Bros Pictures, Universal Studios na Disney Land.
Kanumba pia amep[ata kushinda tuzo mbalimbali kama vile Best actor ya ZIFF, BEST FILM IN SOUND(DEVIL KINGDOM) aliyecheza na Mwigizaji Nguli wa Nigeria Ramsey.
Kanumba
katika vitu ambavyo aliwahi kuvitamka kuwa anavipenda ni watoto nadhani
ndio maana hata katika moja ya filamu zake aliigiza na watoto tu
Jeniffer na Patriki katika Filamu ya Uncle JJ na hivi karibuni aliongeza
mtoto mwingine machachari Sofia.
Pia alipenda kujichanganya na marafiki na kuwa na mitoko kiasi na kupebnda sana kuangalia filamu.
No comments:
Post a Comment