Joseph Ngilisho, Arusha.
CHAMA cha ushirika cha kuweka na kukopa cha walimu katika jiji la Arusha kimeanza
mkakati wa kuwashawishi wanachama wake kununua hisa zaidi ili kukiongeza
mtaji kwa lengo la kuondokana na mfumo
wa sasa wa kutegemea mikopo ya mabenki ambayo wamedai yanatoza riba kubwa
Hayo
yalibainishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyaika sanjari
na kufanya uchaguzi mkuu ambapo mwenyekiti mteule, Theresia Wapalila ameeleza
kuwa hivi sasa wanawaelimisha wanachama umuhimu wa kununua hisa.
Alisema kuwa, hivi sasa ushirika huo una mtaji wa kiasi cha shilingi 500 milioni na
endapo zitaweza kuongezeka kwa wanachama kununua hisa zaidi watakuwa na mtaji
mkubwa wa kukopeshana.
Wapalila
alisema kuwa hivi sasa wamekuwa vwakitegemea zaidi mikopo kutoka katika
mabenki na kukuta chama kikibakiwa na faisa ndogo sana kutokana na riba kubwa
za mabenki.
Kwa
upande wake Makamu mwenyekiti ,Erick Mainowa ameeleza kuwa hivi sasa
wanaandaa mpango mkakati na andiko la mradi ili chama hicho kiwe na njia nyingi
ya kukiongezea mtaji.
Naye
mmoja
ya wanachama wa ushirika huo wa arusha city teachers saccos,Ruth Sabaya
ameeleza endapo watafanikiwa kutatua tatizo la upatikanaji wa mikopo
itakuwa hatua kubwa ya kuwakomboa walimu.
Alisema
kuwa andiko hilo litawawezesha kupa taasisi mbadala na mabenki itakayowawezesha
kupata mikopo ya kuwakopesha wanachama wao wanaofikia 650.
Akifungua
mkutano huo afisa elimu katika halmashauri ya jiji la arusha Anthony Mushi
amewataka walimu hao kuhakikisha wanawekeza katika saccos yao hatua amabyo
itawahakikishia faida kubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment