Friday, May 18, 2012

KUU W WILAYA ZA MKOA WA ARUSHA WAAPISHWA LEO

 mkuu wa wilaya ya Arusha john Mongela akiwa anaapa mbele ya mkuu wa wilaya hivi leo
 Mkuu wa wilaya ya Arusha akiweka saini mara baada ya kuapa
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Manasa akiwa anakula kiapo
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru akiwa anaweka saini ya kiapo mara baada yakumala kuapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha magessa Mulongo
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akiwa anapokea zawadi ya maua kutoka mmoja wa mfanyakazi kutoka ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha
 Mkuu mpya wa wilaya ya Karatu Daudi Mtibenda akiwa anasaini mara baada ya kuapa mbele ya mkuu wa mkoa 
wakuu wa wilaya wa mkoa wa Arusha wakiwa wamekaa kwa pamoja mara baada ya kula viapo wakisikiliza hutuba kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Arusha hivi leo

mkuu wa mkoa wa Arusha katika kati Magesa Mulongo akiwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha aliowaapisha


Baadhi ya wabunge wa majimbo ya mkoa wa Arusha waliuthuria pia


Mkuu wa mkoa wa Arusha  Magesa Mulongo ameyataka mabaraza yote ya madiwani wa mkoa wa Arusha kupitia upya ripoti za mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG) na kuhakikisha kuwa inawachukulia hatrua kali za kisheria watumishi wote ambao ndio chanzo cha hati chafu

 magesa aliyasema hayo wakati akion wakuugea na waandishi wa habari mara baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya  wapya  wa wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha mapema

Alisema kuwa kamwe mkoa wa Arusha haiutaweza kuvumilia utendaji mbovu wa watumishi ambao kila mara wanachangia kwa kiwango cha hali ya juu kukithiri kwa hati chafu wakati hakuna vyanzo vyovyote vile ambavyo vinasababishia halmashauri kuwepo kwa hati chafu

Alibainisha kuwa ili kukomesha tabia hiyo madiwani wote wanatakiwa kukagua ripoti zote na kutokana na hali hiyo hawapswi kuwa na uoga au huruma kwa kuwa hali hiyo ndiyo chanzo kikubwa sana hata cha umaskini.

“leo naawapiusha wakuu wa wilaya na pia napenda kuwataarifu kuwa hakikisheni kuwa kuanzia sasa mnaungana  na madiwani kukagua ripoti hiyo kwa kuwa halmashauri zote zimepata hati chafu kasoro halmashuri ya Meru pekee”alisema  Mulongo

Mbali na hayo alisema kuwa katika halmashuri zote za mkoa wa Arusha kasoro ya Meru kuna mambo makubwa sana ambayo yanaendelea lakini kupitia msaada wa wakuu wapya wa wilaya zote wataweza kusaidia halmashauri hizo.

Bw Mulongo alibainisha kuwa wakuu hao wapya wa wilaya hawapswi kuangalia hekima ya kiongozi ambaye hana maadili na badala yake wanatakiwa kufuata sheria za Nchi kwa kuwa mara nyingine huruma ndiyo inayochangia sana hati chafu

Awali aliwataka wakuu hao wapya wa wilaya kuhakikisha kuwa wanafuatilia masuala mbalimbali ya kijamii hasa pale kwa serikali za vijiji ambazo zinakabiliwa na changamoto kubwa sana

 Mulongo alifafanua kuwa kupitia msaada wa wakuu hao wapya wa wilaya wataweza kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto ya ugumu wa kazi ambao unasababisha watendaji wa vijiji mara nyingi kulazimishwa na wananchi kujiuzulu wakati wapo sawa kwa mujibu wa sheria

Hataivyo katika zoezi hilo wakuu wapya wa wilaya sita za mkoa wa Arusha waliapishwa tayari kwa kuanza kazi za kuwasaidia wananchi katika shida mbalimbali

No comments:

Post a Comment