Thursday, May 24, 2012

Wachimba migodi haramu wafariki


Mgodi Afrika Kusini 

Zaidi ya wachimba migodi 35 haramu wamekwama kwenye mgodi baada kutokea ajali kwenye migodi miwili isiyotumika nchini Afrika Kusini.

Wanaume watatu waliokuwa wanachimba almasi,katika mkoa wa Nothern Cape, walifariki baada ya mgodi wao kuporomoka. Watu kumi na tisa wangali wamekwama kwenye mgodi huo.

Wengine 21 wamekwama katika mgodi wa dhahabu karibu na jimbo la Free State baada ya kuangukiwa na mwamba.

Wote wanasemekana kuwa wachimbaji haramu. Watano waliokolewa kutoka kwenye mgodi, wameshtakiwa kwa kuwepo kwenye eneo hilo kinyune na sheria.

Wachimbaji haramu huhatarisha maisha yao kwa kwenda machimboni mara mingi bila vifaa vya kutosha vya ulinzi

Mgodi huo ulifungwa mnamo aprili.
Watu hao walikuwa miongoni mwa wachimba migodi thelathini waliokuwa wakitekeleza shughuli hiyo wakati mgodi huo ulipoporomoka.

Makundi ya waokoaji yamepelekwa katika kijiji cha mashambani cha Kleinzee na wamekuwa wakijaribu kuwaokoa usiku kucha.

Wakazi wa hapo wamepiga kambi kwenye mgodi huo kusubiri taarifa kuhusu waathiriwa.

No comments:

Post a Comment