Mfalme Abdullah wa Saud Arabia atamzika mrithi
wake,mwanamfalme Nayef bin Abdulaziz leo hii huko
Macca.Mwanamfalme huyo amefariki dunia jana akiwa na umri wa
miaka 79.
Kifo chake kimejiri miezi minane tu baada ya kufariki kwa nduguye mwanamfalme Sultan.Rais Barak Obama wa Marekani ametuma rambi rambi kwa niaba ya wananchi wa Marekani.
Mfalme Abdullah atabidi pia amteuwe mrithi wake mwengine kuiongoza nchi hiyo inayosafirisha mafuta kwa wingi zaidi ulimwenguni.Anaepewa nafasi nzuri ya kumrithi mfalme huyo mwenye umri wa miaka 89 ni mwanamfalme Salman,mwenye umri wa miaka 76 na ambae,kama walivyo wafaleme wengine wote waliopita,ni mtoto wa kiume wa muasisi wa Saud Arabia Abdulaziz ibn Saud.

No comments:
Post a Comment