Wednesday, June 6, 2012

MKUU WA MKOA ARUSHA HAYUPO TAYARI KUFANYA KAZI NA WAKANDASI WASIO WAADILIFU



mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa  Mulongo akiwa anaangalia barabara iliwekwa simeti ikafunikwa kwa ajili ya kuweka lami
 Mkuu wa mkoa magesa Mulongo akiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha
John Mongela wakikagua daraja
wakuu hao wakisikiliza maelekezo kutoka kwa msimamizi wa wakandarasi wa barabara za jijini Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia wakandarasi wa barabara ambao hawajui kazi zao na hawanavigezo kuendelea kutengeneza barabara za mjini hapa kwani wanaweza kuwaletea madhara hapo baadae.
Hayo  yamesemwawakai alipokuwa akifanya ziara yake ya ukaguzi wa barabara mbalimbali zinazojengwa katika kati ya jijini hapa ambapo barabara nyingi zimeonekana kuchibwa na kuachwa na mashimo bila ya kufanyiwa kazi hali inayosababishia jiji la Arusha kuwa na msongamano mkubwa wa magari.
Alibainisha wakandarasi ambao wamepewa kufanya kazi hiyo wamekuwa wanashindwa kufanya kazi ya ujenzi wa barabara kwa wakati kwani tangu wamepewa kazi hiyo wameshindwa kuonyesha kazi waliyofanya kwa kipindi kizima cha miezi saba ambayo wameanza na ndo imemalizika katika kazi hiyo ,na hamna kitu walichofanya wakati mradi huo unatakiwa ukabidhiwe Januari 31 mwakani 2013 kwani ni mradi wa miezi 15.

mulugo alibainisha kuwa iwapo makandarasi huyo ataendelea kufanya vitu hivyo basi wao kama mkoa watafanya apili wao kama serekali na watatuma taarifa kwa benki ya dunia ambayo ndio imetoa fedha hizo za ujenzi wabarabara za jijini hapa kuwa mkandarasi huyo awafai katika kazi kwani anafanya kazi pasipo mipangilio nakujali muda.
"sasa leo tunakuja site na hawa wakandarasi wanajua kabisa twaja miezi saba imeisha hatujaona kitu kinachotengenezwa zaidi ya haya mashimo waliyoyachimba ambayo yanaababishia wananchi wetu kero kubwa kwani hawaoni sehemu za kupita kwa ajili ya mashimo wanasabishia mji wetu kuwa na msongamano wa magari kwa ajili ya wao wanafanya vitu kama hawataki vile sasa nasema sisi tutaapili kama hawatajirekebisha"alisema mulugo.
Aidha mulugo alimtaka mshauri wa mkandarasi huyo ambaye anatoka katika kampuni ya MEERO CO.LTD Eng, Johakimu Bwale asimamie kazi hiyo kwa makini na sio kuifanya kazi hiyo kama mradi wake wa nyumbani kwake na kama ameshindwa aachingazi ili waajiriwe wasimamizi wengine wenye uwezo huku akimtaka apeleke malengo ya kila mradi wa barabara apelekewe matokeo ya mradi huo ,wanaitaji kujua mradi wa mradi na kila mradi unagarimu kiasi gani cha fedha ,barabara imechibwa lini na inatarajiwa kuwekwa lami lini huku akisisitiza wanaitaji mradi huo uishi kwa wakati uliopagwa ili benki hii ya dunia iweze kuwapa fedha za miradi mingine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya arusha John Mongela ambae aliambatana na mkuu wa mkoa katika ziara hiyo ya ukaguzi wa barabara alimtaka mshari wa barabara kutambua kuwa fedha hizo za ujenzi wa barabara ni za serekali na benki ya dunia na sio za kwake za mfukoni huku akimpa ovyo kuwa iwapo ataendelea hivi basi ivi basi atamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumueka ndani .

Alisema kuwa hatakuwa tayari kufanya kazi na watu ambao wanachezea fedha za uma ,akisisitizia kuwa mtu huyo anayefanya hivyo atakuwa salama kata kidogo kwani mtu huyo atakuwa tu anaiba fedha za serekali bali atakuwa anawatesa wananchi ambao wametoa kodi zao .
"unajua sitakuwa tayari kufanya kazi na watu ambao mtaendelea kucheza na fedha za serekali ,kwakeli nasema kuwa hatabaki salama kwani anayefanya hivyo anawaumiza wananchi wetu wewe angalia barabara zimechimbwa mashimo matokeo yake wananchi wanakosa pa kupita msangamano wa magari unakuwepo sitafumbia macho hilo,napia nawaomba meya na madiwani wote wafatilie mradi huu kwa makini kwani ni wawananchi wao wanaumia ni wananchi wao na watakao pata faida ni wananchi wetu ivyo tushirikiane kufatilia"alisema Mongela
Naye mshauri wa wakandarasi hao Johakimu Bwale akiojiwa na mkuu wa mkoa alisema kuwa kazi yao inaenda vyema na wanauhakika kila kitu kitakamilika katika kipindi kilichopagwa japo kuwa muda umeyoyoma ,huku akisema kujwa tatizo lingine lilowafanya kutoweza kujenga barbara kwa haraka ni pamoja na miundo mbimu ya maji machafu ,kwani wanaofia wakijenga mwisho wasiku watakuja kubomoa kwani chema nyingi zimeunganishwa katika barabara hizo huku akiwaondoa viongozi hawa shaka kwa kusema kuwa watahakikisha wanakabidhi bara hiyo

No comments:

Post a Comment