waandishi wa habari wa mkoani Arusha wakiuthuria semina wakiwa na mkurugenzi mtenaji wa UTPC
mkurugenzi mtendaji wa UTPC Abubakari Karsan katikati akiwa anawaonyesha waandishi kijarida chahabari
Waandishi
wa habari jijini Arusha wametakiwa kwenda mashuleni kuongeza elimu ili
kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo ikumba fani hii
katika kipindi hiki pamoja nakijacho
Hayo
yamebinishwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari jijini
hapa(APC)Claud Gwandu wakati akizindua mafunzo ya siku nne ya waandishi
wa habari yaliyoandaliwa nchama hicho kwa kushirikiana na UTPC
yanayofanyika katika ukumbi wa Olasiti jijini Arusha.
Alisema
kuwa ni wajibu wa kila mwandishi wa habari kwenda kuongeza elimu ili
kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukabiliana na
upinzani wa soko la pamoja ambao kutakuwa na wati wengi kutoka katika
nchi mbalimbali wanaofanya kazi hii ya uwandishi wa habari.
Alibainisha
kuwa wanahabari wengi wa mkoa wa arusha wamekuwa wanapuuza kwenda
kusoma kitu ambacho ni kibaya zaidi kwani katika kipindi tunachoelekea
itafikia mahala watu wengi watashindwa kufanya kazi hii kutokana na
kutokuwa na elimu ya kutosha.
Gwandu
aliongeza kuwa waandishi wahabari wanafursa mbalimbali ambazo zinawadia
wao wenyewe kwenda kusoma hivyo ni juhudi ya kila mmoja kujitaidi
kwenda kuongeza elimu.
Alibainisha
kuwa hivi sasa kuna vyuo mbalimbali akitolea mfano vyuo vikuu huria vya
tanzania ivyo ni vizuri kila mwandishi akajiunga katika vyuo hivi kwani
vyuo hivi havibaini mtu kwa sababu vinamsaidia mtu kusoma huku anafanya
kazi.
"hivi
karibuni nimeenda jijini dar es salaam kwakweli napenda kuwapongeza
sana waandishi wa habari wa jijini humo kwani asilimia kubwa nimewakuta
wengi wao kila mmoja anasema anasoma mungine ananiambia anasema
anashahada mungine hiki kweli namefurahi na nawapongeza"alisema Gwandu
Aliwasihi
waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha kuiga wenzao wa jijini dar es
salaam ili na nyie muweze kuendelea ukibainisha kuwa kwa bahati mbaya
katika kipindi hichi ambacho serekali ipo katika harakati ya kupeleka
sera mpya ya habari ambayo wanampango wa kupeleka bungeni.
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa UTPC Abubakari Karsan alisema kuwa
waandishi wa habari wanafursa mbalimbali za kupata elimu ikiwa ni pamoja
na kuandaa miradi na kutafuta wafadhili ambao watawasaidia na mtaweza
kupata fedha za kusomea.
Alisema
kuwa ktika kipindi hichi tunachoelekea mbali na uwandishi kila mtu
anatakiwa kuongeza elimu ili kuweza kujikwamua kimaisha kwani huku
tunapoelekea kama unaelimu basi sio kitu na hauwezi kunufaika kwa kitu
chochote maana wenye elimu ndio watakuwa wanafaidika na wale ambao
hawana wabakia kuteseka tu.
No comments:
Post a Comment