Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesikia harufu ya kuungua kwa
miili ya watu na kuona sehemu za miili imesambaa katika kijiji nchini
Syria ambako mauaji makubwa yalifanyika. Watu 80, wanaripotiwa kuwa
wameuwawa.
Wachunguzi hao hatimaye wameweza kuingia katika kijiji hicho ambacho watu wamekimbia cha Mazraat al-Qubair baada ya kuzuiwa na majeshi ya serikali na wakaazi, na kushambuliwa kwa silaha ndogo ndogo siku ya Alhamis, siku moja baada ya mauaji hayo kuripotiwa mara ya kwanza.
Mapigano Damascus
Katikati ya jiji la Damascus , waasi walipambana na majeshi ya usalama ya serikali siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza , wamesema watu walioshuhudia , na miripuko ilisikika kwa muda wa saa kadha. Majeshi ya serikali , yamelishambulia eneo la kati la mji wa Homs mara kwa mara na majeshi hayo yalijaribu kuingia katika mji huo kutokea sehemu tatu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton amekutana na mjumbe wa kimataifa Kofi Annan mjini Washington kujadiliana nae njia ya kuokoa mpango wake unaolenga lenga wenye lengo la kusitisha umwagikaji wa damu uliodumu miezi 15 sasa nchini Syria.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton
Mataifa ya magharibi yanaulaumu utawala wa Bashar al-Assad kwa
ukandamizaji wa nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali
ambao ulitokana na vuguvugu la maandamano ya umma katika mataifa
ya Kiarabu.Kikosi cha umoja wa mataifa cha waangalizi ni kundi la kwanza huru kuwasili katika kijiji cha Mazraat al-Qubair, kijiji ambacho kilikuwa kinaishi watu wapatao 160 katikati ya jimbo la Hama. Wanaharakati wa upinzani na maafisa wa serikali ya Syria wanalaumiana kwa mauaji hayo na kutofautiana juu ya idadi ya watu waliouwawa.
Taarifa zatofautiana
Wanaharakati wanasema kuwa watu zaidi ya 78, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto wamepigwa risasi, kukatwakatwa na kuchomwa moto hadi kufa, wakisema wanamgambo wanaounga mkono serikali wanaojulikana kama Shabiha, wanahusika na mauaji hayo.
Taarifa ya serikali kupitia shirika la habari la nchi hiyo SANA , imesema kuwa makundi ya magaidi wenye silaha yamewauwa watu tisa wanawake na watoto kabla ya maafisa wa Hama kuitwa na kuwauwawa washambuliaji hao.
Ssusan Ghosheh , msemaji wa kundi la wachunguzi wa umoja wa mataifa, amesema idadi ya watu waliouwawa inayotolewa na wakaazi inapingana na kwamba wanahitaji kufanya uchunguzi wao binafsi wa majina ya watu ambao hawajulikani waliko na watu waliouwawa kwa kulinganisha na orodha inayotolewa na wanakijiji wa kijiji cha karibu.
Harufu ya kuchomwa watu
Unaweza kusikia harufu ya miili ya watu iliyoungua , Ghosheh amesema. Unaweza pia kuona sehemu za miili katika kijiji hicho, ameongeza Ghosheh.
Wachunguzi wa umoja wa mataifa nchini Syria
Ujumbe wa uchunguzi wa umoja wa mataifa umetoa taarifa siku ya
Ijumaa ikisema kuwa alama za magurudumu ya magari yenye silaha
ilikuwa inaonekana wazi katika eneo hilo na baadhi ya nyumba
zimeharibiwa kwa makombora na maguruneti. Ndani baadhi ya nyumba ,
damu ilikuwa inaonekana katika kuta na sakafu, taarifa hiyo
imesema.Wakati huo huo , kiasi watu 12, ikiwa ni pamoja na wanawake wanane , wameuwawa na jeshi la Syria katika mji wa kusini wa Deraa usiku wa Ijumaa, limesema kundi la wanaharakati wanaoangalia hali ya haki za binadamu nchini Syria.
No comments:
Post a Comment