Sunday, June 10, 2012

Mwanasheria wa ICC awekwa kizuizini Libya

Mwanasheria mmoja wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya mjini The Hague ICC amewekwa kizuizini nchini Libya baada ya kukutwa na barua zilizotiliwa shaka alizotaka kuwasilisha kwa mtoto wa Gaddafi alie kizuizini Saif al-Islam.

 Mwanasheria huyo raia wa Australia, Melinda Taylor ni miongoni mwa watu wanne walio katika ujumbe wa ICC ambao walisafiri kwenda mji wa Zintan ambapo Saif al-Islam amekuwa akishikiliwa tangu kutekwa kwake Novemba mwaka jana. 


Mwanasheria mwandamizi katika kesi inayomuhusu Saif, Ahmed al-Jehani amesema wakati alipomtembelea mtuhumiwa huyo mwanasheria huyo alijaribu kutaka kuwasilisha kwake nyaraka hizo ambazo zinahatarisha usalama wa taifa hilo

. Hata hivyo amesema mwanasheria huyo hayupo gerezani, yupo katika nyumba ya wageni na kwamba ataweza kuachiwa huru muda wowote leo hii. 

Upande wa ICC haujazungumza lolote kufuatia mkasa huo. Saif al-Islam ambae anahitajika kwa pamoja na mahakama nchini Libya na ICC alikamatwa na wapiganaji wa Zintan, Novemba mwaka jana katika eneo la jangwa la kusini mwa Libya akiwa amevaa mavazi ya kabila la Bedouin na kumpeleka katika mji wao.

No comments:

Post a Comment