Sunday, June 10, 2012

raia 8 wamefariki dunia katika shambulio

Umoja wa Mataifa umesema raia 8 wamefariki dunia katika shambulio ambalo pia limeuwa wanajeshi saba wa kulinda amani wa umoja huo lililotokea huko kusini mashariki mwa Cote d'Ivoire. 

Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP,  msemaji katika ofisi ya umoja huo inayoshughulika na uratibu wa  masuala ya kiutu, Anouk Desgroseilliers, amesema miongoni mwa raia waliouwawa  ni mwanamke mmoja. 


Walinzi hao wa amani kutoka Niger wameuwawa jana wakati wakipiga doria katika eneo linalounganisha vijiji viwili kufuatia uvumi kwamba kunaweza kuzuka shambulio dhidi ya jamii katika eneo hilo.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani shambulio hilo. Eneo la magharibi mwa Cote d'Ivoire limekuwa na usalama mdogo na kumekuwepo na mashambulizi tangu kuanza kwa mgogoro wa kisiasa na kijeshi mwaka 2010 ambao umesbabisha kiasi ya watu 3,000 kupoteza maisha nchini humo.

No comments:

Post a Comment