Sunday, June 10, 2012

Mapigano yazuka mashariki mwa Libya, watu kadhaa wauawa



Duru za jeshi nchini Libya zimetangaza kuwa, mapigano yaliyotokea kati ya watu wa kabila la Tubus na vikosi vya jeshi la nchi hiyo katika eneo la Kafra kusini mashariki mwa Libya, yamepelekea watu kadhaa kuuawa.
Duru za habari zimemnukuu Issa Abdul Majid mmoja wa viongozi wa kabila la Tubus akisema kuwa, mapema leo asubuhi watu wa kabila hilo walivamiwa na vikosi vya nchi hiyo na kumiminiwa risasi ambapo watu wasiopungua watano waliuawa na wengine 10 kujeruhiwa. Akithibitisha mashambulizi hayo dhidi ya watu wa kabila hilo Wisam bin Hamid kiongozi wa vikosi vya jeshi la Libya amesema, mashambulizi hayo yametekelezwa kama hatua ya kulipiza kisasi kwa mashambulizi yaliyofanywa na watu wa kabila hilo dhidi ya ngome moja ya jeshi la nchi hiyo. 
Amesema kuwa katika hujuma iliyotekelezwa na watu wa kabila hilo dhidi ya ngome hiyo askari watatu walijeruhiwa.
 


No comments:

Post a Comment